Hatma ya uchaguzi mkuu wa TFF kutolewa saa 6 mchana - EDUSPORTSTZ

Latest

Hatma ya uchaguzi mkuu wa TFF kutolewa saa 6 mchana


Hukumu juu ya hatma ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) itatolewa leo Ijumaa Julai 3, 2021 saa 6 mchana na Jaji Edwin Kakolaki.
Mgombea urais, Ally Salehe aliyeenguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi huo katika mchujo wa awali amefungua kesi kupinga muundo na kanuni za TFF katika uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 7, 2021 mjini Tanga.

Baada ya Jaji Kakolaki kusikiliza pande zote mbili kuanzia saa 3:12 asubuhi hadi saa 4:07 asubuhi ameahirisha kesi hiyo hadi saa 6 mchana itakapotolewa hukumu ndogo kama mchakato wa uchaguzi uendelee au la.

Mwanasheria wa Ally Salehe ameiomba mahakama mchakato wa uchaguzi usitishwe kwa muda hadi maombi yao ya msingi namba 305 yatakaposikilizwa.

"Kama uchaguzi hautaahirishwa, kuna uwezekano wa pande zote kupata hasara," amesema Chacha nje ya mahakama.

Mwanasheria wa TFF, Alex Mshumbusi amesema atazungumza baada ya hukumu ndogo saa 6 mchana.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz