Kesi ya Sabaya Kusikilizwa Leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Kesi ya Sabaya Kusikilizwa Leo
KESI za aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano, ambao wanakabiliwa na mashtaka sita na mawili ya ujambazi wa kutumia silaha zitaanza kusikilizwa leo Julai 2.

 

Mashitaka mawili ambayo leo yanatarajiwa kuanza kusikilizwa ni ya ujambazi wa kutumia silaha ambayo mawakili wa Serikali, Tumaini Kwema, Abdallah Chagula na Tarsila Garvas walieleza kuwa upelelezi wake umekamilika.

 

Mashitaka hayo yatafikishwa leo mbele ya mahakimu wawili tofauti; Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha, Katika mashitaka ya ujambazi wa kutumia silaha Sabaya, anayeshtakiwa na walinzi wake wawili wanatetewa na wakili Moses Mahuna.

 

Akiwasomea maelezo ya makosa hayo Juni 18, Wakili Gervas alidai Februari 9, mwaka huu, Sabaya na watuhumiwa wawili, Silivester Nyengu (26) na Daniel Mbura (38) walivamia duka la Mohamed Saad, lililopo mtaa wa Bondeni.

 

Gervas alidai kuwa watuhumiwa hao walitumia silaha, ambayo ni kinyume cha kifungu cha 287(a) cha mwenendo wa makosa ya jinai, kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019. Baada ya kuvamia duka hilo waliwalaza sakafuni, kuwapiga na kuwatishia wa bunduki Bakari Msangi, ambaye ni diwani wa Kata ya Sombetini (CCM) na Ramadhani Khatibu.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz