Cristiano Ronaldo aongoza orodha ya watu matajiri duniani kupitia Instagram - EDUSPORTSTZ

Latest

Cristiano Ronaldo aongoza orodha ya watu matajiri duniani kupitia Instagram
Cristiano Ronaldo anaongoza orodha ya watu matajiri duniani kupitia Instagram, kama mtu maarufu anayetoza gharama ya juu kabisa ya matangazo kuliko mtu mwingine yeyote.
Mshambuliaji huyo wa Juventus anaweza kutoza watu au makampuni yanayotaka kutangaza kupitia mtandao wake wa Instagram mpaka dola milioni $1.6 kwa tangazo moja, hiyo ni kwa mujibu wa Kampuni ya kimataifa ya masoko ya Hopper HQ.

Nyota huyo wa zamani wa Klabu ya Real Madrid, amempiku mwigizaji aliyewahi kuwa mwanamieleka Dwayne "The Rock" Johnson.

Hii ni mara ya kwaza kwa Ronaldo kuongoza kwenye orodha hiyo tangu ianzishwe na kutambulika mwaka 2017.

Mshambuliaji huyo mwenye tuzo tano za mchezaji bora wa dunia 'Ballon d'Or kwa sasa ana wafuasi milioni 308 kwenye mtandao wake wa Instagram.

Johnson, ambaye amekuwa akitamba katika filamu za Fast and Furious, ana wafuasi milioi 250 yeye anaweza kutoza dola milioni $1.52 kwa tangazo moja, wakati nyota wa pop Ariana Grande akiwa nafasi ya tatu akitoza dola milioni $1.51.

Lionel Messi, ambaye wiki hii amekuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Barcelona kumalizika, yuko kweye kumi bora akishika nafasi ya saba kwa kutoza dola milioni $1.1 kwa tangazo. Muargentina huyo ana wafuasi milioni 224 kwenye mtandao wake wa Instagram.

Mshambuliaji wa PSG na Brazil, Neymar ($824,000) ni miongoni mwa wanamichezo wanaofanya vizuri kwenye matangazo akiwa nafasi ya 16.

Kampuni hiyo ya Hopper HQ iliyoko Uingereza, inaendesha akaunti za mitandao ya kijamii kwa niaba ya watu ama makampuni , iianz akuchapisha orodha hiyo ya watu matajiri kwenye mtandao wa Instagram kuazia mwaka 2017.

Baadhi ya vigezo inavyotumia kampuni hiyo kuwapata matajiri hao kwenye orodha yake ni pamoja na kuangalia mtu mwenye wafuasi wengi, kwa kiasi gani anachapsha kweye mtandao wake na anavyoshiriki na kushirikishwa watu wengine kweye akaunti yake.

Tangu mwaka jana wastani wa gharama ya chapisho moja la tangazo kwa Ronaldo, ambaye aliteka vichwa vya habari mwezi Juni kwa kuondoa chupoa za coca-cola kwneye mkutano na wanahabari kabla ya Ureno kukutana na Hungary, zimeongezeka kwa asilimia 54%.

Wako wanawake sita katika oroda ya matajiri hao 10 wa Istagrama ingawa ni kw amara ya kwanza mwaka huu Kardashian au Jenner hawamo kwneye tatu bora.

"Wakati janga la Covid-19 likiendelea na kuathiri maisha yetu, inaonekana kwamba Instagram ndio mahala pekee ambapo haijaathirika na janga, watu wameuwa wakitumia mtandao huo zaidi kuliko wakati mwingine wowote," alisema Mike Bandar,mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Hopper HQ.

"Ni jambo zuri kuona Cristiano Ronaldo akichukua nafasi ya kwanza mwaka huu baada ya kukaa kwenye tano bora kwenye historia ya orodha hiyo'

Orodha kamili watu maarufu 10 wanaoweza kutoza gharama kubwa zaidi kwa tangazo kwenye mtandao wa Instagram

1. Cristiano Ronaldo, wafuasi 308m - $1.6m kwa tangazo (posti)

2. Dwayne "The Rock" Johnson, wafuasi 250m, kwa tangazo

3. Ariana Grande, 247 million wafuasi, $1.51m kwa tangazo

4. Kylie Jenner, 244 million wafuasi, $1.49m kwa tangazo

5. Selena Gomez, 241 million wafuasi, - $1.46m kwa tangazo

6. Kim Kardashian, 232 million wafuasi - $1.41m kwa tangazo

7. Lionel Messi, 224 million wafuasi - $1.16m kwa tangazo

8. Beyonce Knowles, 189 million wafuasi - $1.14m kwa tangazo

9. Justin Bieber, 180 million wafuasi- $1.11m kwa tangazo

10. Kendall Jenner, 172 million wafuasi -$1.05m kwa tangazo

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz