Yusuph Manji atua kwenye mkutano wa Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Yusuph Manji atua kwenye mkutano wa Yanga
Mwanachama na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Yanga Yusuph Manji akiwa na Fransic Kifukwe wamehudhuria mkutano wa mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo ya Yanga ambao unafanyika kwenye ukumbi wa DYCCC


“>Manji amekuwa kipenzi cha wana Yanga kwa muda mrefu na mara kadhaa mashabiki na wanachama wa timu hiyo ya wananchi wamekuwa na hamu ya kutaka kuona anarejea kwenye majukumu ya kuisaidia klabu hiyo siku moja

“>Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka GSM Eng. Hersi Said amesema kuwa anashukuru kuwa sehemu ya familia ya klabu ya Yanga na tayari wameanda fedha kwa ajili ya kufanya usajili wa nguvu, ambao itatufanya kuwa timu bora ndani na nje ya Afrika.

“Wakati tunaingia Yanga tulikuwa na mipango ya mda mfupi na mda mrefu, tunashukuru chini ya mwenyekiti Dr. Mshindo Msolla tumeweza kuinua thamani ya Klabu, mpango wa mda mrefu ni kuhusu mabadiliko ya Klabu yetu ambao haki ya Wanachama wetu imezingatiwa kwa kuwashirikisha,”- Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka GSM Eng. Hersi Said

Katika Mkutano huo Mkuu wa Klabu ya Yanga, umehudhuriwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuph Manji akiwa na Fransic Kifukwe ambapo mgeni rasmi akiwa Rais Mstaafu ambaye pia ni mwanachama Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz