AL Ahly na Kaizer Chiefs kukutana fainali Ligi ya Mabingwa Afrika - EDUSPORTSTZ

Latest

AL Ahly na Kaizer Chiefs kukutana fainali Ligi ya Mabingwa Afrika
MABINGWA watetezi, Al Ahly wamefanikiwa kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Esperance ya Tunisia usiku huu Uwanja wa WE Al-Ahly Jijini Cairo nchini Misri.

Mabao ya Ahly yamefungwa na Ali Maâloul kwa penalti dakika ya 38, Mohamed Sherif dakika ya 56 na Hussein El Shahat dakika ya 60.

Kwa matokeo hayo Al Ahly wanatinga Fainali kwa jumla yaa jumla wa 4-0 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza Jumamosi iliyopita Tunisia. 

Al Ahly sasa itakutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo imeitoa Wydad Athletic baada ya sare ya 0-0 leo Johannesburg kufuatia ushindi wa 1-0 Jumamosi iliyopita Morocco.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz