Kocha Simba: Tunatangazia Ubingwa Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha Simba: Tunatangazia Ubingwa Yanga
SIMBA imepanga kucheza mechi ijayo dhidi ya Yanga kama fainali, huku lengo kubwa likiwa ni kutangaza ubingwa mbele ya wapinzani wao hao wa jadi.

 

Mabingwa hao watetezi, hivi sasa wanahitaji pointi tatu tu kutetea ubingwa wao huo ambapo mechi ijayo ni Julai 3, mwaka huu dhidi ya Yanga.

 

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba inaongoza ikiwa na pointi 73 baada ya kucheza mechi 29, inafuatiwa na Yanga yenye pointi 67 ikicheza mechi 31.

 

Endapo Simba itaibuka na ushindi katika mchezo huo, basi itatangaza ubingwa ikiwa ni mara ya nne mfululizo.Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amefunguka kuwa:

“Tunafurahia kuwa na muendelezo mzuri wa ushindi ndani ya ligi, hii inazidi kutupa hali ya kujiamini kuelekea mchezo wetu ujao dhidi ya Yanga.“Tunatarajia kucheza mchezo huo kama fainali, ili kutangaza ubingwa wetu wa nne mfululizo, tuna michezo mitano mbele yetu na tunahitaji ushindi mmoja pekee, ninaiamini timu yangu na natumaini tutafanya vizuri mpaka mwisho wa msimu.

 

“Kuhusu Chama, huyu ni mchezaji wetu muhimu, anakuwa na mchango mkubwa kikosini, tulipanga kumpa dakika 30 kwa ajili ya kuanza kumuandaa kuelekea michezo ijayo, hasa ule wa nusu fainali dhidi ya Azam na pia mchezo dhidi ya Yanga.

 

”Juzi Jumanne wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbeya City, Chama alicheza kwa dakika 30 akiingia uwanjani dakika ya 60 kuchukua nafasi ya Rally Bwalya.

STORI NA JOEL THOMAS | GPL

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz