DPP Awafutia Shtaka la Utakatishaji Fedha Wakurugenzi wa Bevco - EDUSPORTSTZ

Latest


 

DPP Awafutia Shtaka la Utakatishaji Fedha Wakurugenzi wa Bevco
Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) amewafutia shtaka la utakatishaji fedha  wakurugenzi wa kampuni ya kuagiza vinywaji vikali nchini, Bevco Limited na sasa wako huru kuomba dhamana.

Mapema wakili wa serikali, Ester Martin amedai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya kuwa leo Juni 24, 2021 kesi hiyo ya uhujumu uchumi imekuja kwa ajili ya kuifanyia mabadiriko hati ya mashtaka kwa kuondoa shtaka moja la utakatishaji fedha na kuwasomea washtakiwa mashtaka yaliyobaki.

Katika kesi mpya washtakiwa wanakabiliwa na makosa 48. Lipo shtaka moja la kuongoza genge la uhalifu, mashtaka matano ya kushindwa kulipa kodi, mashtaka saba ya kughushi, mashtaka saba ya kutoa nyaraka za uongo, mashtaka 14 ya kukwepa kodi na shtaka moja la kusababisha hasara kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zaidi ya Sh bilioni 1.6.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Melaine Philipe na Thierry Lefeuvre raia wa Ufaransa,  Joseph Rwegasila aliyekuwa Diwani wa Makongo na Mwanasheria Ntemi Massanja.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Septemba Mosi mwaka 2017 hadi Septemba 2020

Washtakiwa wanadaiwa kwamba kati ya Oktoba mwaka 2017 hadi Juni mwaka 2020 jijini Dar es Salaam, waliisababishia TRA kupata hasara ya Sh 1,658,370,376.29. na kesi imeahirishwa hadi Julia 6, mwaka huu.


Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz