Kasri la angani’’ la Gaddafi latua nyumbani Libya baada ya muongo - EDUSPORTSTZ

Latest

Kasri la angani’’ la Gaddafi latua nyumbani Libya baada ya muongo



Ndege ya kibinafsi ya kiongozi wa zamani wa Libya Hayati Muammar Gaddafi imetua katika katika mji mkuu wa Libya Tripoli baada ya karibu muongo mmoja ikiwa nchini Ufaransa, vimeripoti vyombo vya habari vya Libya na vya Kiarabu.
Ndege hiyo kubwa, aina yaAirbus A340, ilipaa juu ya anga la Tripoli kabla ya kutua katika uwanja wa kimataifa waMitiga karibu na mji mkuu , iliripoti tekevisheni ya Arab Al Arabiya TV.

Vyombo mbali mbali vya habari vilinukuu kauli za Waziri MkuuAbdul Hamid Dbeibah, ambaye alikuwa katika uwanja wa ndege kushuhudia ndege hiyo ikiwasili jana usiku.

Amesema kuwa ukarabati wa ndege hiyo na taratibu nyingine vimekamilika, na serikali ya mpito imelipia gharama zilizohitajika kuirejesha Libya, ilitangaza ofisi ya Waziri mkuu kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Bw Dbeibah alisema kwamba ndge nyingine 14 aina ya jet zilizosalia, 12 kati yake zimepangiwa kurejea Libya, huku serikali ikishughulikia kurejea kwa ndege mbili bora zaidi.

Kulingana na televisheni ya Al Arabiya, jet ya Gaddafi, ambayo inafahamika pia kama"Kasri inayopaa", ilipaa kimo cha chini juu ya mji wa Tripoli na kuyazunguka maeneo kabla ya kutua ardhini.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ndege hiyo, Bw Dbeibah alisema "watu wa Libya ndio watakaoamua hatma yake" na kama itatumiwa na maafisa au wengine, manufaa ya umma, kulingana na Al Arabiya.

Alisema kuwa kurejea kwa ndege hiyo maarufu nchini ni "hatua nzuri kwa Libya, usalama wake na utajiri", ilisema televisheni hiyo.

Ndege hiyo ya kifahari, ilielezewa na baadhi kama " ndege ya Airbus yenye muonekano wa nyumba ya [James] Bond ndani ", ilivivutia vyombo vya habari vya kimataifa kwa miaka iliyopita

Gaddafi – ambaye aliiongoza Libya kwa miongo sita-na ambaye anafahamika kama kiongozi aliyekuwa na nguvu za mamlaka kibinafsi ambaye alionekana katika jukwaa la dunia kama mwenye mtindo wake wa uongozi, aliuawa katika mji wa nyumbani kwa wa Sirte mwezi Oktoba 2011 wakati wa mzozo ulioibuka kufuatia uasi mwezi Aprili mwaka huo.

Mamlaka ya serikali mpya ya Libya, Serikali ya Umoja wa kitaifa(GNU) inayoongozwa na Bw Dbeibah, iliinga mamlakani baada ya kuchukua mamlaka kutoka kwa serikali iliyokuwa na makao yake mjini Tripoli na iliapishwa mwezi Machi kufuatia uchaguzi uliofanyika mapema mwaka huu katika mchakato uliodhaminiwa na Umaoja wa Mataifa.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz