Aliyerekodi Tukio la Kuuwawa Kwa George Floyd Apewe Tuzo - EDUSPORTSTZ

Latest

Aliyerekodi Tukio la Kuuwawa Kwa George Floyd Apewe Tuzo


Bodi ya Tuzo za Pulitzer imempa tuzo ya heshima ya "Pulitzer Prize" na $15,000 (Zaidi Milioni 34 za Kitanzania) Darnella Frazier, Msichana aliyerekodi Video Clip iliyoonesha Tukio la Mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd Mwaka jana Mnamo Mei 25,

@darnella_frazier03 Alikuwa akitembea tu binamu yake mdogo kwenda dukani mnamo Mei 25, 2020, ndipo alipoona mapambano kati ya mtu mweusi na afisa wa polisi Mzungu Akarekodi kwa simu yake Tukio hilo kwa muda wa dakika 10.

Video hiyo ilitumika kama moja ya ushahidi katika kesi dhidi ya Afisa wa polisi, Derek Chauvin na Video yake ilipingana sana na Taarifa ya polisi ambayo ilisema kwamba maafisa waligundua Floyd alikuwa na shida ya kiafya na baada ya kumfunga pingu na kwamba alipelekwa hospitalini kupitia gari la wagonjwa na ndipo alifariki

Kifo cha George Floyd kilisababisha maandamano makubwa ndani na nje ya Marekani yaliyolaani matumizi ya nguvu yanayofanywa na polisi dhidi ya raia pamoja na ubaguzi wa rangi

Tuzo hiyo ya Heshima ya @pulitzerprizes hutolewa kwa watu waliofanya vitu vikubwa na vizuri kwenye jamii






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz