Mfanyakazi wa Ndani Akamatwa Akituhumiwa Kumuua Mama, Wanaye Wawili - EDUSPORTSTZ

Latest

Mfanyakazi wa Ndani Akamatwa Akituhumiwa Kumuua Mama, Wanaye Wawili

 


Dar Es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Shadrack Kapanga (34) kwa tuhuma za mauaji ya mama na watoto wake wawili eneo la Masaki mtaa wa  Maryknol.


Kapanga ambaye ni msaidizi wa kazi za ndani alikamatwa jana Ijumaa Juni 11, 2021 eneo la Magomeni akiwa kwenye harakati za kutoroka baada ya kuwaua  Emilly Mutaboyerwa ambaye ni mama na  Damita (13) na Daniela Mutaboyerwa (15).


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Juni 12, 2021 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu  ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na baadhi ya vitu alivyoviiba baada ya kufanya tukio hilo.


“Vitu alivyokutwa navyo wakati akitoroka ni simu za marehemu, televisheni, king’amuzi cha DSTV na rimoti,” inaeleza  sehemu ya taarifa hiyo.


Muliro ameeleza kuwa upelelezi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la mauaji Juni 9, 2021 baada ya kuwapiga kila mmoja kwa wakati tofauti kwa kitu kizito na kuwasababishia kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.


“ Baada ya kuwaua aliwafungia ndani na kutoroka. Upelelezi wa shauri hili unaendelea ili kujua sababu za msingi za mauaji hayo na mara utakapokamilika mhusika/wahusika watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo,” inaeleza.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz