ADUI MKUBWA KATIKA MAHUSIANO - EDUSPORTSTZ

Latest

ADUI MKUBWA KATIKA MAHUSIANO

 

Kuna maadui weeeengi wametuzunguka ndani ya ndoa zetu na kama hatukupambana nao hatuwezi kua na utulivu Wa nafsi hata siku moja.
Leo naomba tumuangalie adui namba moja anaitwa
"DHARAU"
*Dharau* na kutokujali ni maadui pacha wanaofuatana,hakuna binadamu anaependa kudharauliwa hata aweje,kila mmoja anahitaji kuona cheo chake kwa mwenzake.
*Dharau* ni donda sugu linaloondosha uhai Wa ndoa zetu kila kukicha.
👉Mwenzako amekukataza kitu hujali........
👉Mwenzako amekushauri kitu hujali.......
👉mwenzako anaumwa hujali.....
👉mwenzako amepata matatizo hujali.....
👉mwenzako ameomba umfanyie kitu hujali....
👉mwenzako anaongea nawe hata humuangaliii wala humsikizi......
👉mwenzako anachukia kitu ndio unafanya maksudi....

Hizo ndio *dharau* na kuonesha dharau hata kwa wazazi na ndugu Wa mwenzako.
Tujaribu kuwafukuza kwenye nyumba zetu maadui hawa *DHARAU* na *KUTOKUJALI* na badala yake tuwakaribishe *KUJALI* na *KUBEMBELEZA*
Hebu anza kumuonesha mwenzako kua unamjali na unajali hisia zake, anapoongea nawe acha yote mskize kwa umakini hata kama hufurahii analosema ,mshauri kwa lugha ya upole ,muoneshe upendo na tabasamu mda wote, akikosea mfahamishe kistaarabu hakuna mkamilifu hata wewe pia unamkosea.
May be an image of 1 person and standing


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz