Faida zitokanazo na kufanya mapenzi pekee - EDUSPORTSTZ

Latest

Faida zitokanazo na kufanya mapenzi pekee


Pata GB 10 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kufanya mapenzi ni jambo muhimu sana katika mahusiano. Huwakutanisha na kuwaweka pamoja wewe na mpenzi wako. Mapenzi hulifanya penzi lenu kuwa hai.

Kufanya mapenzi ni kichocheo muhimu cha kuamsha hisia zenu za kimahaba. Hii ni mada kuu inayopendwa na huongelewa sana na wanaume pamoja na wanawake.

Ni kitu ambacho kila mtu hukifikiria hata kama hawako katika hali ya mapenzi. Kwa kweli ni muhimu tu kama uaminifu na mawasiliano.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwa nini kufanya mapenzi ni muhimu katika mahusiano;

Hukuza urafiki baina yenu na kuimarisha mahusiano.
Kuwa na mpenzi ambaye ni rafiki yako ni jambo zuri sana katika mahusiano. Kuwa katika mahusiano pasipo kufanya mapenzi na mwenza wako ni kama tu kuwa na rafiki yako. Mahusiano hujawa na uchu, wapenzi hutaka furaha na kuridhika. hivyo kufanya mapenzi na mwenza wako huchochea hisia nzito baina yenu, huburudisha na kuyafanya mahusiano kuwa bora.

Huondoa mawazo
kufanya mapenzi husaidia kuondoa mawazo, ufanyapo mapenzi homoni zinazokupa furaha hutengenezwa kwa wingi mwilini. Kumbuka unapokuwa na furaha ndivyo unavyoweza kufanya kazi kwa ufanisi.

Huyafanya mahusiano kuwa hai.
Kujamiiana ni kitu ambacho unaweza kufanya ili kujifurahisha wewe pamoja na mwenzi wako. Hukuza urafiki na kuwa na hakika, vile vile huwafanya mujione kuwa kila mmoja anahitajika na mwenzake.

Kufanya mapenzi ni njia nzuri ya kuwasiliana, huwafanya mpendane zaidi na kuuona umuhimu wa kila mmoja katika maisha yenu ya mahusiano.

Hukufanya uwe na usingizi mwanana.
kufanya mapenzi hukufanya ulale usingizi mzuri. Siyo kwa sababu ya uchovu wa shughuli nzito mliyoifanya. Unapomaliza kufanya mapenzi kemikali iitwayo ‘oxytocin’ huachiwa na mwili. Hii hukufanya kulala usingizi mzuri na wa raha.

Hukupa furaha.
Watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na furaha zaidi ya wale wanaofanya mara chache au wasiofanya kabisa. Vile vile hukuongezea kujiamini na kuwa na mtazamo chanya katika maisha.

Humpa furaha mwenza wako.
Kufanya mapenzi huwafanya wanaume wanapokuwa na msongo wa mawazo, kujisikia furaha. Kama uko kwenye mahusiano na huwa hamfanyi mapenzi mara kwa mara, kuna hatari kuwa mwenza wako hapati furaha 100%. Hivyo kama hamtofanya mapenzi, kuna uwezekano wa yeye kwenda kutafuta mtu mwingine wa kufanya nae mapenzi. Hivyo ili kumfurahisha ni vyema muwe mnafanya mapenzi mara kwa mara.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz