MWANAMAMA AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA MAPENZI NA MIZIMU 20

MWANAMAMA AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA MAPENZI NA MIZIMU 20


Anaitwa Amethyst Realm mwanamke kutoka Uingereza, amewahi lalamika katika kipindi cha Televisheni cha ‘This Morning’ cha ITV ya Uingereza kwamba amefanya mapenzi na zaidi ya Mizimu 20.

Anasema kisanga kiliamza mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 15 ambapo yeye pamoja na familia yake walipohamia katika nyumba mpya na baada ya siku chache akaanza kuhisi mtu anamshikashika usiku huku hamuoni na kupelekea kufanya nae mapenzi, hali iliyodumu kwa takribani miaka 14 .

Anadai ilianza kama nguvu fulani hivi inampapasa, baadae akawa anaona kabisa anahemewa mihemo maeneo ya shingoni na anashikwashikwa sehemu za mwili wake usiku bila kumuona anaemshika na baadae wanafanya mapenzi.

Hali hii anasema ilimtokea kwa miaka mingi hadi siku moja alipomtembelea mpenzi wake na wakati mpenzi wake alipokuwa anarudi nyumbani usiku alikuta kivuli kinakimbia kupitia dirishani na akahisi alikuwa na mwanaume ndani na hapo ndipo ilikuwa mwisho wa mahusiano yao.

Licha ya kumwambia mpenzi wake asihangaike kumtafuta mwizi wa penzi lao kwa sababu kamwe asingempata kwakua hakua mtu wa kawaida bali ulikuwa ni mzimu, kitu ambacho hakikuweza kumuingia akilini na kuamua kuchukua hamsa zake.

Anaeleza kwamba alikuwa anahisi ladha ya penzi huku anaemfanyia haonekani na alikuwa amefanya mapenzi mara nyingi sana na mizimu tofauti zaidi ya 20, hadi anafanyiwa mahojiano hayo mwaka 2017 anasema alikuwa amekwishapata ujauzito kwa njia hiyo na alionyesha kuridhia kuendelea na mahusiano yake na mizimu.

“Ni kweli mzimu hauwezi  kuninunulia maua au kunitoa kwenda sehemu kufurahi lakini furaha ninayoipata kwake ni isiyo na kifani, naota Ndoto nzuri na najihisi furaha“, alisema Amethyst.

“Wakati wa tendo nahisi miguso na raha ya ajabu huku anaenifanya simuoni na kuna muda hua nashangaa nageuzwa kabisa kufanyishwa mapenzi mitindo Tofauti tofauti.  Nimewahi sikia mara nyingi juu ya jambo hili la mwanamke kulala na viumbe wasioonekana usiku na sasa ninahisi nina ujauzito wa viumbe hao”

Hiki ni kisa cha kweli ambacho kimemtokea binti huyu raia wa Uingereza na hali kama hizi huwatokea watu wengi, wanawake kwa wanaume japo wengine kusema hawawezi.

Previous Post Next Post