UNAJUA NI KWANINI KWENYE NDOA AU MAHUSIANO YA KAWAIDA INAFIKIA TIME MWENZA WAKO ANAKUCHOKA TU TENA BILA SABABU?? HEBU SOMA HAPA UJUE ZAIDI - EDUSPORTSTZ

Latest

UNAJUA NI KWANINI KWENYE NDOA AU MAHUSIANO YA KAWAIDA INAFIKIA TIME MWENZA WAKO ANAKUCHOKA TU TENA BILA SABABU?? HEBU SOMA HAPA UJUE ZAIDI

Kuna wakati mwingine katika ndoa na katika mahusiano ya kawaida inafikia mwenza wako anakua anakuchoka tu. Hana hata sababu anakua kakuchoka, sasa anapokuchoka hata kama hamuwezi kuachana lakini kumbuka kuwa unavyozidi kujipendekeza ndiyo unavyozidi kumboa, anaanza kukuona kama kero. Labda nikupe mfano, una rafiki yako ananuka mdomo, huwezi kumuambia kuwa unanuka mdomo kwakua ni rafiki yako unaogopa kumuumiza.
Lakinio pia hutapenda aongee mbele yako, na hata akiongea basi utasogeza pua yako pembeni? Sijui kama unanielewa, sasa chukulia huyo rafiki yako anakuona unasogeza pua pembeni yeye ndiyo anajileta kabisa, anaongea mbele yako tena na vimate aanatoa, si unaweza hata kumtandika makofi? Sasa kuna watu wako hivyo, wapo kwenye mahusiano, washachokwa wanaboa lakini ndiyo kwanza wanakua ving\’ang’anizi na kujifanya kujali, kuonyesha ujuzi na kumganda mtu mpaka inaboa!
Sasa unatakiwa kufanya nini ukiwa katika hali hii, turudi katika yule rafiki yako mnuka mdomo, anachotakiwa kufanya badala yua kung’angania kuongea na kujitia kiherehere kuwa anajua kila kitu basi anatakiwa kupiga mswaki na kujipulizia manukato anukie ndiyo wewe ambaye unaona hupendwi mapenzi yamepungua na kila unachomfanyia kinakua kero, hembu ondoka kapige mswaki hapa ni kwakuanza kujipenda wewe, uwe na furaha wewe kabla ya kumpeleke mdomo wako.
Jipulizie manukato kwa kujifanyia mambo yanayokupa furaha, ndiyo maana nakuambia basi kasome Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” sehemu ya nne. Jipende wewe, jifurahishe wewe yaani kwa kifupi kapige mswaki uone kama hatakuja kwako na mate atataka! Lakini ukiendelea kung’ang’ania kumfurahisha yeye kama si makofi atakukimbia kabisa. Bei ya Kitabu ni Shilingi elfu kumi tu, unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 kama unataka watu wakufurahie basi anza kujifurahia mwenyewe.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz