UMEPISHANA NA GARI LA MSHAHARA WAKATI UKIKIMBIZA GARI LA MAJI MACHAFU! - EDUSPORTSTZ

Latest

UMEPISHANA NA GARI LA MSHAHARA WAKATI UKIKIMBIZA GARI LA MAJI MACHAFU!


Naomba nisaidie, nahisi X wangu ameniloga, ni kweli nilimkosea, nilikutana na huyu Dada wakati sina kazi, yeye ahajasoma ila alikua anafanya bisahra, akanichukua mpaka kwake, akaniweka kwenye Biashara zake basi nikazifanya kisomei mpaka tukafungua kampuni, lakini nilimdananya nikaandika majina yangu na dada zangu. Baadaye nikaja kuona kuwa si wa hashi yangu, tukaachana nikaenda kuoa mwanamke mwingike.
Wakati naachana na huyu dada nilikua nafanya bishara mzunguko mpaka milioni mia tano kwa mwaka, ila tangu nioe ni mwaka wa pili sasa yaani sina kitu, kampuni nimefunga, mke kanikimbia na ndugu hawanitaki. Nimeenda kwa waganga naambiwa huyu dada ndiyo kanifunga, nimemtafuta nataka hata kurudiana naye hataki, nimemuomba aniachie lakini hataki, ila najua anakusoma na rafiki yake ananiambia anakuamini sana, naomba unisaidie ili hata kama hataki turudiane basi aniachie niwe na maisha yangu kwani hata kupata kazi sipati.
JIBU LANGU; Hakuna mtu aliyekuloga bali nikwakua umesoma ila hujaelimika, kuna watu wana akili za darasani na kuna watu wana akili za maisha, wewe una za darasani kukariori na si kutafuta maisha, huyo mwanamke uliyemuacha alikua na akili za kutafuta maisha, alikutengeneza wewe ulipopata ukadhani ni kwakua una kili ukamsahau bila kuja kujua kuwa huyo mwanamke alikua ni Injini, basi ukabadilisha injini ya gari, ukadhani litatembea.
Hiyo ni sababu ya kwanza ya wewe kufeli, sababu ya pili ni kwakua katika maisha kuna watu wana bahati zao tu, kwamba kila wakigusa kitu kinafanikiwa, anekugusa wewe umefanikiwa na kuna watu wana magundu yao tu, kila wakigusa kitu basi ni mkosi, sasa wewe una gundu lakondiyo maana ulipogusa maisha ya dada wa watu ukayaharuibu, ukakutana na mtu mwenye ngekewa ukafanikiwa, badala ya kumtumia vizuri ukachukua na ndugu zako ambao nao wana gundu kama wewe.
Kabla ya huyo dada nao walikua hawana kitu basi ukaoa na mwanamke mwingine inawezekana ana nyota kama yako kisha ukamfukuza mwenye ngekewa yake na sasa imekula kwako! Pole lakini sidhani kama huyo dada anatakiwa kukurudia, pambana na hali yako utatoka, na najua kabisa kama ananisoma nahisi ashaiva hawezi kufanya ujinga huo, hujalogwa ndugu yangu, kilichotokea nikuwa, umepishana na Gari la mshaara wakati ukikimbiza Gari la maji machafu!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz