MWANAMKE YAISHI MAISHA HALISI KULINGANA NA VILE ULIVYO WALA USIFUATE USHAURI WA MTU AMBAYE KWA MACHO NI KAMA AMEKAMILIKA AKIFICHA UHALISIA WAKE💯 - EDUSPORTSTZ

Latest

MWANAMKE YAISHI MAISHA HALISI KULINGANA NA VILE ULIVYO WALA USIFUATE USHAURI WA MTU AMBAYE KWA MACHO NI KAMA AMEKAMILIKA AKIFICHA UHALISIA WAKE💯


Watu wengi wana-fake life!
Na ukitaka kuchunguza maisha yao wanakukwepa ili usije ona mateso yao, Kwa macho na masikio yako utasikia WALIVYO FANIKIWA KUWA NA MAHUSIANO AMA NDOA NJEMA japo kwa uhalisia sio kama wanavyoonekana😂😂
Paa za nyumba🏚 zimesitiri watu wengi sana, Unakuta Mtu ameolewa na anaishi kwa msemo wa AFADHALI YA JANA ila akitoka nje utadhani hana matatizo🤔
nawe usivyo na akili UNAMWAGA MATATIZO YA NDOA YAKO HAPO ukiamini utapata suruhisho la matatizo yako kumbe unayemwambia matatizo yako ni MSIRI yake haweki hadharani ila anayo makubwa kuliko ya kwako😂
Mahusiano ama ndoa ni jambo la watu wawili, Mtu wa tatu hana nafasi na kama atakuwepo basi hapashwi kuwa SABABU YA MAELEWANO YENU kwani ninyi ndo mtajua MAKOSA NA KUYASAHIHISHA kuliko kuyaweka wazi kwa Mtu kama mkishindwa wenyewe mnalo jukumu la KUPEANA NAFASI MPYA💯
Mahusiano au Ndoa ni zao la MAPENZI hivyo ifahamike kama ulivyo usiri wa FARAGHA ndivyo anapashwa kuyalinda mahusiano na ndoa yako💪
Wewe hujui lini aligombana na MWENZA wake ila wewe hata ukikosa mboga tu kiguu na njia kuanika ya kwako, Janga hili ni lenu wanawake kwani ukikuta Mwanaume ametoa siri ya mkewe ujue huyo ni FALA📌
Wanawake mnaangamia kwa kukosa MAARIFA kwani unakwenda kwa Mwanamke mwenzio kunadi ubaya wa mumeo na hapo ndipo atatofautisha ubaya wa Mumewe na Mumeo usije shangaa akamtaka mumeo kwani wako ameonekana ana nafuu kwani Matatizo yanatofautiana kulingana na uhitaji wako mwenyewe, na hapo ndo chanzo cha kuimba kale ka wimbo ka #Shaa;
• SHOGA YANGU HATA WEWEEEEE♪♫♬
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria 🔨
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz