DADA ZANGU NAOMBA NIWAKUMBUSHE HILI. - EDUSPORTSTZ

Latest

DADA ZANGU NAOMBA NIWAKUMBUSHE HILI.

Dada bado nawakumbushia, ukijua kuwa mume wako ana mtoto nnje ya ndoas, kabla ya kupigia simu ndugu, kupigia msahoga zako, kupata povu na kumuuliza mwanaume basi jiulize swali moja tu. “Hivi naweza kumuacha huyu mwanaume kwakua ana mtoto?” Kama jibu ni Ndiyo, basi kaa kimya miezi miwili kisha muulize mume wako, na kisha muache rudi kwenu!
Lakini kama jibu ni hapana, huwezi kumuacha basi baki kimya, yaani jifanye kama hujui khata kama mume wako akitoka huko nnje mbegu zake zinafanya kazi. Lakini ukimuuliza mwanume kuna mawili, akatae basi ubaki na kisirani chako, au baya zaidi akubali, akuombe msamaha, umsamehe au utishie kuondoka urudi kwennu wiki, kisha uchukue na Shangazi kaja lako urudi.
Ukishamsamahe basi jua kuwa, atamhudumia mtoto wake kwa uhuru, hutaweza kumpangia namna ya kumhudumia, muda wa kuongwa na Mama wa mtoto, kumpangia amchukue mtoto au asimchukue, kumpangia alipe ada au la. Utaishia kuonge, akitaka atafanya, kuondoka hutaondoka.
Yaani hii kitu ni sawa na Muisalamu anyekula kiti Moto, yaani wengi wanafanya kwa kificho, huwezi kujua akiona tu Bucha atalaani mpaka basi, ila, ukishajua kuwa mshikaji anakula basi atakula kwa uhuru, wakati mwingine atataka mpaka umpe lift au umnunulie, afiche nini tena wakati ushajua, yaani ipo siku hata atakuja kukukope pesa mtoto anaumwa na usipotoa atakuona una roho mbaya!
Nishamaliza, ila si mnajua nikiandika kuna mtu yashamkuta, tena wawili walikua wananisoma, wakelewa, wakatoa na Povu, wakapovuka kuwa wakwangu nikijua namuacha, basi yamewakuta wamechunguza hata msamaha hawajaombwa wametulia tu wamesamehe kimoyo moyo hawana namna! Mwanaume akishajua huondoki basi jua anakua na uhuru hata wa kumleta mtoto na utaishia kulia tu kindanindani!
Kama huwezi kumaucha basia cha kuulizia, haikuongezei chochote!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz