SOMA HII HALAFU NIAMBIE UMEJIFUNZA NINI? - EDUSPORTSTZ

Latest

SOMA HII HALAFU NIAMBIE UMEJIFUNZA NINI?


Mwanamke na mwanaume walikuwa wakiendesha magari tofauti, yakagongana. Magari yote yakaharibika vibaya kwani ajali ilikuwa mbaya na ilisababishwa na uzembe wa mwanamke.
Pamoja na magari yao kuharibika vibaya cha kushangaza kati yao hakuna aliyeumia. Walipojivuta kutoka kwenye magari, mwanamke akasema,
"Wewe ni mwanaume!...inafurahisha sana, na mimi ni mwanamke. Angalia magari yetu, hakuna kilichobakia lakini bahati nzuri hakuna aliyeumia. Lazima hii ni ishara kutoka kwa Mungu kwamba tuwe marafiki na tuishi pamoja kwa siku zote za maisha yetu zilizobakia".
Mwanaume akajibu,
"Nakubaliana na wewe kabisa. Lazima hii ni ishara kutoka kwa Mungu".
Mwanamke akaendelea "...na angalia huu muujiza mwingine, gari yangu imeharibiwa vibaya, lakini chupa hii ya mvinyo (wine) haikuvunjika. Kwa kweli, mungu anataka tunywe mvinyo huu na kusheherekea tulivyo na bahati nzuri.
Mwanamke akampa Mwanaume ile chupa. Mwanaume akainamisha kichwa kutoa ishara ya kukubali. Mwanaume akaifungua na kunywa nusu ya mvinyo na kumrudishia mwanamke.
Mwanamke akachukua chupa, akafunga kizibo haraka na kumrudishia tena mwanaume.
Mwanaume akauliza "Haunywi hata kidogo?"
Mwanamke akajibu "Hapana, nadhani nitasubiri POLISI waje kuchukua ushahidi wao (KOSA LA DEREVA KUENDESHA GARI HUKU AMELEWA)."
UMEJIFUNZA NINI?
1. Adam amekula tunda tena!
2. Wanaume hawajifunzi kamwe!
3. Wanawake hawabadiliki!
Molito Brand 

WHATSAPP 0716528779
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz