MY STORY; KATIKA MAPENZI HAKUNA KULIPA KISASI UKIACHWA ACHIKA! - EDUSPORTSTZ

Latest

MY STORY; KATIKA MAPENZI HAKUNA KULIPA KISASI UKIACHWA ACHIKA!


Image may contain: 1 person
Mwaka 2017 ndiyo nilikutana na ukurasa wako, nilikua kwenye mahusiano na Kaka mmoja ambaye alikua ananisumbua, kila siku nilikua namfumania na wanawake naishia kupigwa na kumuomba msamaha. Rafiki yangu ndiyo alinielekeza kwako, nilinunua kitabu chako na kukisoma, baadaye nilikupigia ukaniambioa kuwa huyo mwanaume hawezi kunioa kwani mimi si wa hadhi yake.
Uliniambia nimemzidi elimu, nimemzidi pesa na hajiamini. Nilikuuliza inamaana watu waliozidiana elimu na pesa hawaoani? Uliniambia hapana, wanaoana ila inahitajika mwanaume ajiamini, kwamba mwanaume aamini katika uanaume wake, kwamba asijihisi anhanyanyaswa, asjidharau ndiyo ndoa uitasimama. Uliniambia huyo mwanaume ananipenda lakini kwakua hajiamini basi hana akamani.
“kila dakika anahisi unamdaharau, yaani hata ukijamba atahisi unamdharaau kwakua hana pesa kumbe tumbo linamuuma. Chunguza, huyo mwanaume sio kama anachepuka tu bali ana mwanamke mwingine ambaye anamaisha naye ila hawezi kukuacha kwakua anakupenda.” Kweli kaka nilichunguza nikakuta kuna mwanamke kampangishia nyumba wana mtoto na anahudumia kila kitu.
Kusema kweli nilipojua nilimuuliza, alinitukana sana na kuniambia kuwa ni bora tuachane niondoke, alinipiga sana, nikaamua kuondoka na kuchana naye. alimuoa huyo mwanamke miezi miwili tu baad aya kuachana naye, alinitukana sana, akanitangazia ubaya na kuniambia kuwa sitakuja kuolewa kwani nampenda sana siwezi kupata mwanaume mwingine.
Kwakua nakusoma nilijipa moyo, nililia lakini nilitulia na maisha yakaendelea, mwaka 2018 niliingia kwenye mahusiano na Kaka mmoja, yeye alikua ananipenda na ananijali, nikawa na furaha tena, mwezi wa tisa mwaka 2018 huyo Kaka alikuja kujitambulisha kwaajili ya ndoa. Kaka nimekuja tena, baada ya kusikia nina mchumba kaja kujitambulisha X wangu akaja kwakasi na kusema kuwa alioa kwa hasira ila ananipenda mimi.
Mimi tayari nilikua nakusoma nikasema siwezi kurudiana naye, tukawa tunachart tu ila kwa bahati mbaya mwezi wa 12 nilijikuta narudiana naye, aliniahidi kuwa anataka kumuacha mke wake kwaajili yangu. kwakua nakusoma nilijua kabisa kuwa huo ni uongo nataaka kunichezea, lakini nilikua na hasira naye kama ambavyo aliniumiza nilitaka kumuumiza, nilimuambia kuwa kweli na mimi nampenda na nipo tayari kumuacha mchumba wangu kwaajili yake.
Wakatai huo alikua ananisikiliza na kufanya kila kitu ninachokitaka, nilimuambia kuwa kama ananipenda kweli basi anininunulie kiwanja, nilijua kabisa hana pesa kwa wakati huo kwani alikua nanalalamika, lakini alienda na kuuza kiwanja cha mke wake ambacho walikua wanajenga akanipa ile pesa kama milioni saba na mimi nikanunua kiwanja changu.
Kusema kweli nilijisikia vizuri kwani alishakula pesa yangu nyingi sana na kuniumiza sana, nilikua simpendi na nilikua nafanya hivyo ili kumuumiza. Mwaka jana mwezi kwanza nilipata ujauzito wake, nilikua najua kabisa kuwa mimba ni yakwake na nilimuambia kabisa kuwa nina mimba yake. Alifurahi sana na kuniambia kuwa yupo tayari kuja kwetu na nisitoe mimba yake, nilimkubalia kuwa sitakuja kuitoa lakini sikua na mpango wa kuolewa naye.
Mchumba wangu naye alipojua basi alifurahi na kulazimishia kuwa tuoane kwani ananaipenda sana, nilikubali kwakua alishajitambulisha na kutoa mahari ntulifunga ndoa mwezi wa tatu. Yule Kaka hakuamini kuwa nimemuacha na kuolewa na mwanaume mwinmgine, alinitafuta sana na kunisumbua lakini nilimuambia kuwa simtaki kama yeye alivyoniumiza basi na mimi nimeamua kumuumiza.
Alinisumbua sana akawa mpaka anamtafuta mume wangu, kwa bahati nilishamuambia mume wangu kuwa nina X wangu ananisumbua na jkila nikikutana na huyo mwanuame basi nilikua nafuta meseji zangu wkenye simu yake hivyo hakua na ushahidi wowote. Waliishia kutukananana na mume wangu mpaka akakata tamaa, akazidi kunitangaza ila mimi sikujali nilikua kwenye ndoa yangu na nilikua na furaha.
Mwezi wa tisa mwaka jana nilijifungua mtoto wakiume, hapo ndiyo kila kitu kilianza kubadilika. Baada tu ya kujifungua X wangu alianza kunitafuta kuwa anataka mtoto wake, mimi niligoma kabisa na kumuambia kuwa huyo mtoto ni wamume wangu na nilimdanganya yeye kwakua nilikua nataka kumuumiza. Kumbe wakati naongea naye alikua ananirikodi akamtumia mume wangu na kumuambia kuwa mtoto ni wangu.
Mume wangu aliniambia nikalazimika kumuambia kuwa ukweli kuwa kuna kipindi nilirudiana na X wangu lakini si kwa mapenzi bali nilitaka tu kumuumiza. Kaka tangu hapo mwanaume haongei na mimi, hahudumii chochote, hajanifukuza lakiniu hataku hata kumgusa mtoto analazimisha kuwa tukapime DNA kwanza ili ajue mtoto ni wahani? X wangu naye anasema anachotaka ni mtoto basi ila yeye hanitaki, naomba ushauri wako Kaka nifanye nini wkani najihisi kuchanganyikiwa!
MWISHO
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz