Kati ya fikra zinazowasumbua sana baadhi ya wanawake ni kujiambia kwamba sihitaji kumilikiwa au kumtegemea mwanaume kwasababu ninajitosheleza, ninauwezo, naweza kujitegemea. Sihitaji mtu wa kuwa baba wa watoto wangu maana ninaweza kulea mwenyewe. Fikra hizi zimewaumiza wanawake wengi kihisia ingawa huwa hawasemi ukweli, maana ukweli ni kwamba hatuingii kwenye mahusiano kwa ajili ya vitu tu, na hatuingii ili kuchukua tu. Maranyingine tunaingia ili kutoa, tunaingia ili kushare, tunaingia ili kushirikiana. Nivema ufahamu kwamba kunavitu zaidi ya vile unavyodhani wewe kwenye mahusiano. Ukishakuwa na mtazamo mgando basi unajiweka kwenye mazingira ya kuumizwa na kulalamika kila siku
#Alenno
#Alenno
No comments:
Post a Comment