HIVI MTU ALIYE KWISHA ZAA au KUZALISHA HANA HAKI YA NDOA ?? - EDUSPORTSTZ

Latest

HIVI MTU ALIYE KWISHA ZAA au KUZALISHA HANA HAKI YA NDOA ??


Kwa nini MWANAMKE aliye kwisha zaa anapewa nafas ndogo sana ya kuolewa kuliko mwanaume mwenye mtoto??
Kabla hujamunyoshea kidole Mama mwenye mtoto ila hana mume kwanza jiulize mazingira ya yeye mpaka kukaa peke yake na mtoto.
Sio kila mwanamke mwenye mtoto bila mume basi ukajua alikuwa MALAYA. Kuna mwingine alijitunza sana ila siku yake ya 1 kushirik tendo la ndoa ndo sku hiyo hiyo alipata mimba na ika kataliwa. Sasa huyu utamlaum kwa lipi??
Kuna ambae Aliolewa na akazalishwa ila mume akawa msumbufu hatimaye ndoa ikavunjika mume kaoa mke mwingine ...lakin yupo ambae mwenye mimba alikubali kuwajibika ila baadae ana mgeuka mama na mtoto..
Sasa kwa nini mwanamke mwenye mtoto ionekane ajabu kuolewa kwake wakat huo huo mwanaume mwenye mtoto ionekane kawaida kuoa mke wa kumlelea mtoto wake??
"Mimi siwezi KUOA mwanamke mwenye mtoto..kwanza ntaanzaje kulea damu isiyo yangu?? Ulishawah ona wapi mechi haijaanza ila timu moja ina goli??"
"Mimi sijawah zaa sasa ntaanzaje kulea mtoto wa mwanamke mwenzangu?? "
Hayo huwa maneno yetu wanaume pale tunapo potoshana vijiweni..ila jiulize
1.sawa hutak kuoa mwenye mtoto..lakin we ni wangap uliwapa mimba umewakataa na wamezaa??
2.unasema huwez lea damu ya mwenzako..je mkeo saiz ana mimba au mtoto .una uhakika gan kuwa mimba ilikuwa yako?? Wanaume weng siku hiz wanalea damu zisizo zao bila kujua
3.kama huwez OA mwenye mtoto sasa kwa nini una wapenz weng tena wenye watoto zaid ya 1???
4: kuwa na mwanamke aliye kwisha zaa ila ana jiheshimu na ana akili ya maisha au kuwa na bint mrembo aliye toa mimba za kutosha afu ana tembea na vibabu vyenye pesa kipi bora??
Mtazamo wangu
Kuishi na mtu ambae tayar alisha zaa awe mwanamke au mwanaume sio kosa
Kosa ni pale ambapo ameoa au kuolewa ila bado ana mawasiliano ya karibu sana tena kimapenz na mzaz mwenzake huku wakisingizia kujadili malez ya mtoto.
Wasi wasi huja pale : " nikizaa mtoto wangu ntaanza kukitesa kitoto chake.......Akinizalia damu yangu ntamwambia mtoto wake aende kwa baba yake"
Kumbe ukiridhika na MWANAUME/MKE mwenye mtoto ziba masikio ishi nae kikubwa mheshimiane na kupendana. Tena kuna wakat mtoto asiye damu yako mukimlea vizur anaweza kuwa msaada kwako kuliko matikiti unayo dai damu yako...nawe kama mwenzako amekubali kulea damu isiyo yake mheshimu na kuwa na msimamo..Aliye kukimbia asije kulaghai akiona unapendeza....
Kuna watu wanaishi pamoja kwa furaha mpaka huwez amin kuwa kuna mtoto wa kambo ktk familia ile...
Usitangulize fikra za matokeo mabaya mengine mwachie MUNGU atakae kuongoza... Hakuna anae jua maisha yake ya kesho yatakuwa vipi...Unaweza jikuta unampoteza mume bora na kuangikia kwa muuza sura Play Boy kisa tu yule bora ana mtoto aliye za na mwanamke mwingine...utampoteza mwanamke sahihi ila ukaokota kahaba....
Fanya maamuz sahihi kwa wakat sahihi kuepuka majuto kesho. Tabia ikawe kigezo kikuuu ktk kuchagua mwenza sahihi. Uzazi sio ugonjwa.. Ielewe vyema kauli hii
PENDA UA na BOGA
Sio kila MREMBO/MTANASHATI anafaa kwa ajili ya ndoa..wengine wapo ili kuharibu na kuchelewesha malengo ya wenzao .maisha yako ya kesho yatajengwa na maamuz yako ya leo. Usipende fuata kila wazo la ndugu au rafik maana sio utakao ishi nao milele
Kaka au dada una mtoto ipo sku utapata mzaz mwingine kisha mtaongeza wengine. Uskate tamaa kwa mawazo ya wachache ya kukatisha tamaa..
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz