Fahamu Vitu Hivi Mwanaume Anavyokupima Kujua Unafaa Kuolewa Au Ni Hit And Run - EDUSPORTSTZ

Latest

Fahamu Vitu Hivi Mwanaume Anavyokupima Kujua Unafaa Kuolewa Au Ni Hit And Run

1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa tu, so wewe ujiongeze.

2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakutest aone kama utasema "Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu".

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia "Baby twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia". Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!!

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!!

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio tule wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana.

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.

9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe 
niBongofleva, Hip Hop, Diamond, Davido na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi.

11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia. Marks hizo




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz