HAWALA NI ZAO LA MAKOSA YA MUME/MKE NDANI YA MAHUSIANO/NDOA ILIYO INGIWA MIGOGORO 💯 - EDUSPORTSTZ

Latest

HAWALA NI ZAO LA MAKOSA YA MUME/MKE NDANI YA MAHUSIANO/NDOA ILIYO INGIWA MIGOGORO 💯


Mahusiano ama ndoa iliyoshiba UPENDO huyachukulia makosa kama sehemu ya kujisahihisha, kuliko kuchukulia makosa kuwa sehemu ya fimbo ya mkosaji.
Kama MIGOGORO ingedhibitiwa kwa kutafuta SURUHU hakuna anayehitaji KUWA NA WATU WAWILI KAMA WAPENZI huku tayari anae ampendaye⛔️
Kama SURUHU haitapatikana kipindi cha joto la MIGOGORO kwenye mahusiano au ndoa kitu pekee kinachoweza kuleta ukombozi kwa kipindi hicho ni MAJIBU YA UPOLE kinyume chake ni njia mbaya inayompeleka Mwenza aliyekata tamaa kwa tafuta FARAJA NJE YA MIGOGORO HIYO💯
Ndo maana nikasema;
• HAWALA NI ZAO LA MAKOSA.
Tiba pekee wakati wa MAKOSA kwa Mwenza wako ni MSAMAHA na kuonyesha UNAJUTIA ULICHOMKOSEA mwenzio, Kwa sababu hakuna Mtu awezaye kumtibu Mtu aliyeumia tofauti na aliyemuumiza japo wengi wetu akiumiza anajaribu kujihesabia haki wala hajali alichokifanya kwa mwenza wake.
Mtu aliyeumia ni rahisi kutekwa ki mahaba na HAWALA kwa sababu ndogo sana;
• ANAHITAJI FARAJA ILI KUONDOA MAWAZO MABAYA YALIYOTAWALA AKILI YAKE.
Hawala anajengwa na Makosa ya Mwenza anaweza kuendelea kushika nafasi NZURI KWA MHANGA WA MAUMIVU YALIYOTOKANA NA MWENZA au Mkosaji akajisahihisha na kurudi kusema NISAMEHE NILIKOSEA NA SINTORUDIA TENA automatically HAWALA hatakuwa na nafasi kwani ili HAWALA apatikane maana yake MMILIKI wa mahusiano ama ndoa yupo kwani asingekuwepo asingeitwa HAWALA ILA ANGEITWA MMILIKI💯
Kama unampenda MPENZI AU MKE/MUME usitafute FARAJA nje yake bali kaa nae ujaribu kuweka wazi yanayokuumiza, Ni kweli inawezekana haingiliki kutafuta SURUHU ila kuamua kutafuta Mtu ili awe PIPI WAKATI WA NYONGO KUJAZA MATE MACHUNGU MDOMONI haimaanishi ndo suruhu yake
Bali unaweza kutafuta njia sahihi KUNYAMAZA na kuji-cancel mwenyewe na kama MAHUSIANO AMA NDOA hiyo hataweza kuwa kama ulivyotarajia JUST LEAVE kuliko kuwa na watu wawili kwani HAWALA HAWI MBABE KWAKO ila uhakika wa UPENDO WAKE KWAKO NI BAHATI NASIBU pengine maumivu yako yalijawa udhaifu ukaonekana unahitaji FARAJA wala huna UPENDO nae mwisho kabisa nae ni KUKUTUMIA WEWE💯
Siku zote Mapenzi ya kuiba ni matamu kuliko ya uhuru kwa sababu moja tu;
• MAPENZI YANAHITAJI MAANDALIZI YA KI AKILI NI RAHISI MNO KUSIKIA RADHA UITAKAYO.
Na ukiishazoea penzi la kuiba wallah MKE AU MUME hataweza kukupa utakacho japo inawezekana penzi lake lazidi penzi la HAWALA ila issue ni MAANDALIZI YA KI AKILI kwani wana MAHUSIANO na wana NDOA wengi tunaishi kwa mazoea hata ile hali ya BASHASHA HUTOWEKA na hapo ndo maana HAWALA HUPATA NAFASI KUBWA KULIKO MWENYE MKE/MUME.
#Elista_kasema_ila_sio_sheria 🔨
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz