Mwanamke mfahamu Mwanaume MUOAJI ili ujitenge na kuingia kwenye Mtego wa NDOA usiyoitarajia; - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwanamke mfahamu Mwanaume MUOAJI ili ujitenge na kuingia kwenye Mtego wa NDOA usiyoitarajia;


• MWANAUME MWENYE TAMAA YA NGONO HAWEZI KUWA MUME
• MWANAUME ASOKUWA NA KIPATO CHAKE MWENYEWE HAWEZI KUWA MUME
• MWANAUME ASIYEJUA HAKI ZA MWANAMKE HAWEZI KUWA MUME
Maana ili Mwanaume awe MUME anawajibika KUITUNZA FAMILIA YAKE💯
Ni kweli MAPENZI huota popote lakini fahamu kwamba ANDALIO LA NDOA NI LA MWANAUME na kama Mwanaume anakuja kwako kwa tamaa ya ngono huwezi kujivunia nae kwani HAMU ZAKE ZIKIISHA hutaweza kuiona FURAHA NA AMANI iliyokuvuta kwake.
Mwanaume anapokuja kwako ili uwe mke wake huku hana kipato ATAKUTUNZAJE? Wakati huo huo Mwanaume anayekuja kwako ili akuchukue kama Mke wake halafu hajui haki zako kama Mke unatarajia kuwa NA AMANI MAISHANI MWAKO?
Yote na yote KUMDEKEZA MWANAUME HUKU UKIJUA MAJUKUMU YAKE KWAKO ni kuandaa ugonjwa ambao wewe mwenyewe hutaweza kuutibu 😂😂
Mwanaume muoaji ni yupi?
• MWANAUME MUOAJI NI YULE ANAYEAMUA KUWA NA MWENZA WA MAISHA YAKE ILI WAJENGE FAMILIA ITAKAYO KUWA NA MAHITAJI STAHIKI 💯
Na Mwanaume huyo lazima ajitenge na TAMAA YA KI MAUMBILE KWA MWANAMKE kwamba atamuoa Mwanamke ambaye hana muonekano wowote ili akamtunze apendeze aendane na Muonekano autakao Mwanaume kwa mkewe.
Mwanamke ukiolewa na Mwanaume anayekuja kwako kwa MSHAPE wako vipi maisha yakienda kombo? Mwanamke unaolewa na Mwanaume anayehitaji ulezi wako kwake vipi ukiishiwa? Jiulize Mwanamke anakuja Mwanaume awe Mumeo halafu hajui HAKI ZAKO KAMA MWANAMKE hujiulizi kama hatakuwa MWENYE HEKIMA kwako utaangamia?
Mwanaume ameumbwa na TAMAA💯
Lakini ili tamaa ya Mwanaume ipate heshima ni pindi anapokuwa ANAMTAMANI MKEWE maana yake ile PACKAGE OF LOVE  ishamiri na kumfanya Mwanamke kufurahia NDOA yake kwani ili MWANAMKE AWE NA BUBUJIKO LA FURAHA KWENYE NDOA YAKE NI PAMOJA NA MWANAUME KUMALIZIA HAMU ZAKE KWA MKEWE.
Yote na yote USIMFUGE MUME bali tafuta PAKA WA KUFUGA ATAKULA PANYA😂😂
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz