HAUWEZI KULAZIIMISHA PENZI" - EDUSPORTSTZ

Latest

HAUWEZI KULAZIIMISHA PENZI"


usimfikirie mtu ambae hana ata mda wa kukufikiria... yaani wakati wewe ikiumiza kichwa kumfikiria yeye anafikiria kazi, familia yake, X wake na mengine ambayo ni kwa faida yake, usipoteza nguvu zako kwa mtu ambae ata hajibu msg zako kwa sababu kila akisoma ulichoandika anaona kama huna jipya, unapoteza hisia zako na mda kwa mtu mtu ambae hata haoni thamani yako na Bado unajipa tumaini kwamba ni wako? Penzi ni kitu ambacho hakiwezi kulazimishwa kwani nature ya penzi ni UTASHI.... inaweza kutokea au haiwezekani kutokea na kama ikitokea inatokea kwenye mkonyezo wa jicho pamoja na ishara ya mikono kwamba umeguswa nae lakini hilo halimaanishi kwamba LITADUMISHA FURAHA YENU! Upendo ni kitu ambacho hauwezi kuomba au kuendelea kuomba Mtu akupende bali anaweza kukupenda kwa hiyari yake, Kwa hiyo kama mtu asiporudisha upendo wako kama ambavyo binafsi yako unajua UNAMPENDA basi ujie PENZI LENU NI LA UPANDE MMOJA NAO NI WEWE PEKE YAKO.... usimpe umuhimu kwenye maisha yako Mtu ambaye yeye mwenyewe hajui umuhimu wako wala hajui umuhimu wa penzi lenu, usipoteze hisia zako kwa mtu asiethamini upendo wako wala kujua kama unampenda bali yeye anachukulia kama kitu cha kuondoleana uchovu wa kiuno, Mtu ambae uwepo wako au kutokuwepo kwako hajali na ukiondoka ni kama hukiwepo na ukiwepo ni kama haupo UNANGOJEA NINI KWA MTU KAMA HUYO? Usichukie watu ambao wanakuhitaji tu wanapotaka kitu kwako Kwani Kuna thamani unayo ndo maana wanatamani usiondoke, We ni wa muhimu pia ikiwa unajijua kwamba WAPO ULIOWAKATAA NA WALILIA KWA AJILI YAKO... Lakini usije kukubari AKILI ama MOYO wako ukamfuata uliyemliza kwa sababu umeona mahala ulipo hapakufai ATAKUADHIBU ujutie wala usije kujua utaponea wapi, Bin adam wana tabia za kulipiza maana uliumiza moyo wake tarajia maumivu, kwa hiyo usitoe hisia zako au mda wako kwa mtu ambae ata hazihitaji pengine hitaji lake ni mwili wako na sio utu wako, usipoteze machozi yako kwa mtu asie yathamini yaani ukilia anakuona kama MTU ANAELIA KWENYE THAMTHILIA LA KI-NIGERIA😂 kama hawarudishi upendo wako kwa upendo WAFUTE AKILINI WAKO! tena si uhusiano halisi kwa Mtu ambaye anahitaji kukutumia kwa haja zake, upendo haupangwi wala kujadiliwa, kama watu wawili wamemaanishwa kuwa pamoja hawatakiwi kulifikiria au kulifanyia kazi bali inatokea tu... hakutakuwa na machozi wala mitafaruku kwenue penzi ambalo yeye mwenyewe anashauku ya kukuona siku zote, ni upendo tu ndo wenye kuweza kuleta wawili kuwa kitu kimoja, hicho ndo unachostahili mwenye UPENDO kwamba apewe kipaumbele kwenye JAMIII, UKOO, FAMILIA pamoja na MARAFIKI... Ukiona huwekwi hadharani yaani "UNAFICHWA" Ujue yupo aliye huru💃kwahiyo toka na ukatafute UHURU! Penzi lenye Uhuru lina AMANI NA FURAHA...
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz