WANAWAKE TAMBUENI HILI - EDUSPORTSTZ

Latest

WANAWAKE TAMBUENI HILI


Image may contain: 1 person, standing

Wanawake tambueni hili. Ukiolewa na mwanaume ambae anasikiliza matakwa ya wazazi wake jinsi ya kuishi na wewe jua upo gerezani sio kwenye ndoa.
Ukiona Mume wako yupo tayari hata wifi zako wakuingilie kukufokea na kukutukana halafu ukimweleza ananyamaza jua wewe hujaolewana na huyo mwanaume wewe ni mjakazi wa familia.
Ukiona kila wakati mama wa Mume wako anakutembelea halafu wakati mwingi mumeo anakuwa bize na mama yako halafu mambo yanabadilika jua mume wako anachukua ratiba ya kuishi na wewe kwa mama yake.
Ukiona mkikosana tu na mumeo anakimbia kuwaambia wazazi eti wakuite wakuonye kuhusu mmm nakuonea huruma kwa kweli upo kwa shida.
Wanaume kuweni na akili Mungu alijua sababu ya yeye kusema hivi.
Mwanzo 2:24
Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Mungu alithubutu kusema mwanaume ataachana na wazazi lakini mume asimwache mkewe mpaka kifo.
Umeshawahi kujiuliza kwanini?
Mungu anajua watu wenye uwezo mkubwa wa kuharibu ndoa ni wa upande wa familia ndio maana akasema lazima uachane na wazazi wako uungane na mkeo nanyi mtakuwa sio wawili tena ni mmoja.
Yaani mwanaume mwenye akili timamu akioa lazima ajitenge na watu wa familia yake na kumlinda mkewe kwa garama yoyote maana ninyi ni mmoja sio wawili tena.
Wapo wanaume wanawasikiliza wazazi wao kuliko mke wake na hata wakiambiwa wacha mkeo wapo tayari kabisa na hili ni chukizo kwa Mungu na kukosa akili.
Wamanaume wengine ni hatari utakuta anadiriki kukaa na dada zake na wazazi wake wakimsengenya mkewe,
yaani yeye atakachoambiwa na familia anaona sawa tu hata haangalii ni lipi jema na bila kuwa na ufahamu wa kujua mkewe ni mwili wake.
Yaani wapo wanaume hata bila sababu yoyote aliyo nayo kwa mkewe akiambiwa tu huyu mke wako hafai kwenye familia yetu anasikiliza tu na kumfukuza mkewe.
Yaani anaamini watu wa familia yake kuliko mkewe ambae ndie mwili wake. Kwani uliolea familia? Nauliza.
Yuko tayari kuongea madhaifu ya mke wake bila kuwa na ufaham kuwa hafai kumfunua mkewe na pale anafunuliwa anapaswa kumfunika.
Wakati mwingine wanalaumu wanawake ndio wanawatenganisha na wazazi lakini sio kweli huwa wanachoshwa na kejeli na masimango ya familia alikoolewa.
(Ingawa wapo wanawake wa namna hiyo)
Nimeshuhudia hata wanaume waliooa mke hapati mtoto tu hata mwaka haujaisha ameanza kusutwa na mumewe kuambiwa mfukuze.
Na wanafanya hivyo bila kujua jambo hilo Mungu ameliona na umejiletea laana kwa familia yako hata kama utapata watoto mia moja.
Najaribu kutafakari tu.
Mimi nilipomuoa Mke wangu nilitambua vyema japo familia yetu inamuhusu sikuwaolea wao nilimuoa awe wangu.
Na ndie nitaishi nae mpaka kifo kitutenganishe. Ninachokifaham bibilia imetuambia tuwaheshimu wazazi wetu na hiyo ahadi ina miaka nyingi na heri hapa duniani.
Lakini hawaruhusiwi kuingilia ndoa ya watoto wao hata kidogo na huo itakuwa ni uchokozi na hawaruhusiwi kuchokoza watoto wao.
Sasa najaribu kutafakari ile miaka yote niliishi na mke wangu 15 bila watoto nisingekuwa na ufahamu huo wa neno la Mungu,
Kuwa imenipasa kuachana na baba yangu na Mama yangu niambatane na mke wangu ingekuwaje?
Nadhani msomaji jibu unalo. Pengine mke wangu angekutana na mambo ya ajabu yanayowatokea wengi kwa wale bado wanafikiri wanaolea wazazi wao.
Na pengine ningeshawishiwa mambo ambayo yangesababisha nimtende mke wangu mambo ya hiana japo Mungu hapendi.
na pengine tuachane maana sote tunajua vishawishi vya familia vilivyo kwa wale wasiokuwa na ufahamu na Mungu.
Lakini mke wangu nilimpenda na ninampenda tena sana na ninamjali kumlinda na kumtunza kama rafiki na msaidizi wangu wa karibu kuliko wote Yesu akichukua nafasi ya kwanza.
Na kwa jinsi hiyo niliweza kuvumilia na kumwamini Mungu huku nikionyesha upendo wangu kwa mke wangu mpaka Mungu alipokuja kutupa watoto wawili.
Na sasa tumeingia mwaka wa 20 wa ndoa yetu na hakuna siku hata moja wazazi wetu waliwahisikia jambo lolote baya kwenye ndoa yetu.
Ingawa hakukosi kupitana kwa sehemu lakini tumejifunza kuombana msamaha na kamwe hatujaruhusu mtu yeyote kujua mahali tumewahi kupitana,
Kiasi cha watu wengi kuulizaga hivi sisi huwa tumewahikukosana kweli? Na tumemweka Mungu mbele kuliko mambo yote na ndie ametuwezesha.
Kweli kumcha Mungu na kuliishi neno lake ni ufahamu.jina la Yesu libarikiwe.
Sio vibaya ikiwa wazazi wanaweza kukushauri jambo jema linaloweza kuwasaidia kama wanandoa lakini sio kuwachonganisha na hata kuwatenganisha au kuingilia uhuru wenu.
Lakini sio kuingilia mkeo na kumtukana na kumfanyia vioja na kibaya mwanaume mzima na ndevu zako ukiangalia tu eti kisa ni wazazi wako.
Yaani wanawake niwaambie ukweli na hili mlitambue.
Ukiolewa na mwanaume anaependa wazazi wake na kuwaamini na kuwasikiliza kuliko wewe umekwisha jua utakuwa ndani ya gereza sio ndoa.
Ukiolewa na mwanaume anaepangiwa jinsi ya kuishi na mkewe na wazazi wanaonekana wazi bado wana mamlaka ya kumwongoza mumeo jua upo gerezani.
Na asilimia kubwa wazazi ni upande wa mama mkwe na mawifi ndio wabaya zaidi na wenye ushawishi mkubwa kuliko hata baba mzazi.
Wengine wanapigwa kutukanwa mpaka na mawifi zao huku wazazi wakikazana huyu hatufai mwanaume mzima na ndevu zake anaangalia tu!
Halafu mwanaume kama huyo ikimfika shingoni akutane na rafiki zake utasikia akiwaambia naona nitaachana na mke wangu aisee.
Akiulizwa kwa nini utasikia wazazi wangu hawampendi. Akiulizwa sababu utasikia sijui aisee yaani hawampendi tu.
Nauliza tena. Ikiwa wewe ni mwanaume wa aina hiyo uliolea wazazi wako au mke ni wako?
Ni vizuri tukatambua kuwa ukiolewa au ukioa umekuwa na wazazi wa pande zote mbili na unastahili kuwaheshimu na kuwatunza.
Lakini hawaruhusiwi kuendeleza utawala wao tena kwenu kwa jinsi yoyote kuingilia uhuru wenu ninyi ni familia nyingine inayojengwa na watu wawili waliopendana wakaacha wazazi wao na kuungana pamoja.
Ndoa nzuri ni ile inajengwa na watu wawili kwa upendo na Mungu akiwa ndie mjenzi mkuu ndoa hiyo utaifurahia hakika.
Hivyo ikiwa wewe ni mwanaume wa aina hiyo badilika usikubali wazazi au dada na ndugu zako kumwingilia mkeo.
Mpende mkeo kumlinda kumjali na kumtunza huyo ni mwili wako na ndie msaidizi wako na hakuna rafiki wa Muhimu maishani mwako kama mkeo.
Ukijua wengine kwa kusikiliza wazazi wao na kuwanyanyasa wake zao na wengine kuachana leo hii wanajuta kwa shida wanazopitia usiambiwe hiyo ni laana.
Kumbuka ili Mungu akubariki ni lazima umweshimu mkeo kumpenda kumjali na kumtunza kama mwili wako utamfanya awe mke mwema kwako na kupata kibali kwa Mungu.
Kumbuka kibali cha kupata baraka za Mungu kipo kwa mkeo na wengi bila kujua sasa wamefilisika na kuhangaika na wengine kuishi maisha magumu sama soma hii.
Mithali 18:22
Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.
Hivyo tambueni hilo na ni vizuri kutambua bila Yesu ni kazi bure kwa kuwa neno la Mungu linasema hivi.
Zaburi 127:1
BWANA asipoijenga nyumba
Waijengao wafanya kazi bure.
BWANA asipoulinda mji
Yeye aulindaye akesha bure.
Tafakarini hayo chukua hatua utaona matunda yake na utayafurahia.
Wenu
Pastor
Filbert
Lekule.
Nawapenda upeo
Mbarikiwe
Share na wengine na Mungu atakubariki hakika
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz