BINTI YANGU NAOMBA USOME HII. - EDUSPORTSTZ

Latest

BINTI YANGU NAOMBA USOME HII.


💘"Mama anaongea na mwanawe na kumpa Usia"​
💘Mwanangu mpenzi:
💘Kuna siku utanikuta uzee, sitafanya mambo yangu kwa akili;
💘Yakitokea hayo nakuomba tafadhali nipe muda na subira ili unifahamu !!​
💘Pale mikono yangu itakapo tetemeka, na chakula changu kikaangukia kifuani pangu, na nisipoweza kuvaa nguo zangu;
💘Jifunge na kusubiria, na kumbuka miaka imepita nilikuwa nakufunza ambayo leo siwezi kuyafanya!!​
💘Ikiwa leo si maridadi na sina harufu nzuri; usinilaumu.. kumbuka udogoni kwako nikijitahidi sana nikufanye uwe maridadi mwenye harufu nzuri!!
💘Usinicheke utakapoona ujinga wangu na kutofahamu mambo ya wakati wenu huu, lakini wewe kuwa jicho na akili yangu ili niyapate niliyoyakosa!!
💘Mimi ndiye niliyekufunza adabu na mimi ndiye niliyekufunza vipi ukabiliane na maisha;
💘Sasa leo unanifundisha yaliyo wajibu na yasiyo wajibu? ni kwa vile nimezeeka.
💘Usinichoke kwa udhaifu wa kumbukumbu yangu, na uchelewaji wa maneno yangu na fikra zangu wakati ninapozungumza nawe, kwani furaha yangu wakati huu ni kuwa pamoja nawe tu!!
💘Wewe nisaidie tu kupata ninachohitaji; kwani bado najua ninachotaka!!
💘Miguu yangu ikikataa kunipeleka sehemu ninayotaka kwenda; nihurumie na kumbuka kwamba mimi nilikushika sana mkono ili uweze kutembea!!
💘Usione haya abadan kunishika mkono wangu leo; kwani kesho utatafuta wa kukushika mkono wako!!
💘Katika umri wangu huu; elewa kuwa mimi siyaelekei maisha kama wewe; lakini kwa ufupi nangojea mauti; kwa hiyo kuwa pamoja nami wala usinitupe!!​
💘Pale ukikumbuka makosa yangu; jua kuwa mimi nilikuwa sitaki ila maslahi yako!!
💘Na mimi napenda sana unayonifanyia hivi sasa kwa kunisamehe matelezo yangu na kusitiri aibu zangu..​
💘Bado vicheko na tabasamu zako vinanipa furaha kama ulivyokuwa mdogo... kwa hiyo usininyime suhuba yako!!
💘Nilikuwa nawe wakati unazaliwa; jitahidi kuwa karibu nami pale nitakapofariki!!​
💘💘NAWE MOLA AKUGHUFIRIE NA AKUSTIRI!!💘💘
💘Maneno bora yaliyopitia katika maisha yangu, na hata nikiyarudia mara elfu moja, sichoki kuyasoma.."Mola wangu warehemu wazazi wangu kama walivyonilea nilipokuwa mdogo.
💘MANENO MAZITO KWA MWENYE AKILI💘
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz