MKASA WA KUSISIMUA: AMA KWELI MWANAMKE MPUMBAVU HUIVUNJA NDOA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE - EDUSPORTSTZ

Latest

MKASA WA KUSISIMUA: AMA KWELI MWANAMKE MPUMBAVU HUIVUNJA NDOA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE


No photo description available.
#inasikitisha

"Yuko wapi? Yuko na mwanamke mwingine? Inakuwaje ameniweka hapa muda mrefu hivi? Mke mwenye hasira alikuwa akijiuliza wakati akimsubiri mumewe.
Mahusiano yake na mumewe hayakuwa mazuri kwa miaka kadhaa tokea wafunge ndoa. Ndoa yao ilikuwa imezungukwa na wasiwasi, tetesi, uvumi na vita baridi.
Alikuwa akihitaji sana kurekebisha kasoro zilizopo ili Ndoa yao iende vema, ndio maana alikuwa ameandaa chakula cha usiku kwa ajili ya kula pamoja na mumewe ili wasuruhishe matatizo yao.
Alikuwa ameandaa mishumaa iliyotoa mwanga hafifu wa mahaba, akapika chakula kizuri akipendacho mume wake.
Lakini ni saa nne kasorobo hii mume wake yuko wapi? Na huku alimuahidi atawahi kurudi wayasuruhishe!
Dakika 56 baadae, bado hajaingia nyumbani. Akaamua ampigie simu.
"Hallo" sauti ya mwanamke ilisikika kutoka upande wa mumewe.
Mwanamke akapandwa na ghadhabu, mwanamke mwingine ana simu ya mumewe?
"Wewe ni nani unaongea na simu ya mume wangu?" Mke alifoka katika simu.
Akajibiwa;
"HAWEZI KUONGEA NA SIMU YUPO ANANISHUGHULIK......."
Simu ikakata, akajiuliza huyu mwanamke anaoongea na simu ya mume wangu amenikatia simu au nini!!
Mke akajaribu kupiga tena, lakini simu ya mume wake ikawa imezimwa haipatikani.
Mume wangu yupo anamshughurikia?
Mke akashindwa kuvumilia kabisa. Akampigia simu yule kijana ambae amekua akimtongoza kila siku aje pale nyumbani kwake na kumueleza kuwa mume wake hayupo.
Yule kijana ambae amekua akimtongoza hakupoteza muda, alitoka nduki fasta utafikiri fisi ameona mfupa na akasema ama hakika mbuzi amefia kwa muuza supu.
Jamaa alipoingia tu ndani, mke akiwa na hasira akamvua nguo jamaa kama hana akili vizuri huku akijiambia kuwa kama mumewe anaweza kutembea na wanawake wengine huko nje na yeye anaweza hivyo hivyo.
Kijana ambae amekuwa akimtongoza kwa muda sasa, akakipata kile alichokua akikihitaji tena zaidi maana hajatumia hata gharama. Mke alifanya mapenzi kwa hasira. Na akasema hicho ni kisasi cha mumewe kumsaliti.
Kila walipokua wakiendelea kufanya mapenzi alikumbuka sauti ya mwanamke aliyepokea simu ya mumewe na hasira zikazidi kumpanda na kuendelea kufanya mapenzi.
Baada ya muda kidogo mume aliingia ndani, na akapokelewa na ushuhuda mke wake akifanya mapenzi na mwanaume mwingine.
Maua na boksi la zawadi alilokua amebeba mume vikaanguka chini.
Kijana akakimbilia suruale yake, kukwepa kupigwa Nakozi na mume wa yule dada. Akafanikiwa kukimbia huku ameshika suruali mkononi.
Mke? Alikuwa amelala palepale akiwa uchi wa mnyama!
"Ni nini kinaendelea hapa?" mume aliuliza kwa ghadhabu na kutoamini.!
"Ndio, hupaswi kunilaumu, kama wewe unaweza kufanya mapenzi nje ya ndoa usifikirie kuwa mimi siwezi, mke alimwambia mumewe huku akijifunika na mtandio.
"Ni nini? Mimi ninafanya mapenzi nje ya ndoa? Nani amekuambia hilo?" mume alifoka kwa ghadhabu.
"Nani ameniambia? Nani ameniambia?" mke akafoka pia kwa mumewe.
"Unarudi nyumbani kwa kuchelewa, rafiki zangu wanakuona. Nimekupigia kukukumbusha kuhusu kikao chetu cha leo, ni nini nilichokisikia? Sauti ya mwanamke mwingine akiniambia upo unamshughurikia. Unamshughurikia nini? Hutosheki kwangu? - Mke aliendelea kufoka kwa hasira
Mume akashangaa mno, "Hivi ndivyo kumbe, hivi ndivyo vinavyosumbua ndoa yetu? Wewe ni mrahisi sana kuamini maneno ya watu na mawazo yako hasi kuliko mimi mume wako. Ok sawa, amini wanayokwambia, lakini ngoja nikwambie ukweli.
Kazini kwangu kuna wanawake wazuri wengi tu. Wanajipendekeza kwangu lakini mimi sijipendekezi kwao, wananisumbua sana lakini nimekuwa na msimamo siku zote. Ninakuongelea sana wewe mbele yao hata kama ninawaudhi, ninavaa pete ya Ndoa kwa majivuno.
Mume akaendelea.
"Ndio unaniudhi, ninachukia kurudi nyumbani kwa sababu ya ugomvi na maneno kila siku, unaanzisha ugomvi kwa kila kitu. Asipige simu mtu au kuingia meseji katika simu yangu basi ugomvi.
Nina bet kwamba hao marafiki zako, hao marafiki zako wanaokulisha uzushi wana wivu; wana wivu baada ya mimi kukuoa wewe. Nashangaa umeangukia katika uongo wao, Niambie rafiki yako yupi ameolewa?
Umewaacha wameshinda sasa, wamekulisha hadithi za kufikirika na umekuwa sadiki, umewaamini. Hawanijui mimi vizuri na kiundani, lakini wewe unanijua.
Ulipaswa kufahamu kuwa nakupenda , nachukia kugombana na wewe kila siku. Hua natamani nikae ofisini mpaka saa sita usiku. Nirudi nikukute ukiwa umelala ili tusigombane. Nachukia mno ugomvi.
Mke akatizama maua na boksi la zawadi vilivyoanguka chini .
Mume akafuta machozi yaliyokuwa yakimlenga na kusema, "Nilifikiri tumekubaliana kumaliza tofauti zetu, nilikuwa nawahi kuja kwenye kikao chetu cha usuruhishi; nilikuwa nimekununulia maua na zawadi ya necklace.
Nikiwa njiani, nikaona mwanamke mjamzito akihangaika kufungua tairi la gari lililopata pancha. Nikaona si vibaya nikimsaidia, simu yako ikaita kwa kuwa nilikuwa nimechafuka mikono nikamwomba aitoe mfukoni mwangu.
Nilipoona call yako nikamwambia apokee akwambia nimepata emergency nasaidia kubadilisha tairi la gari la ndugu hapa barabarani. Bahati mbaya simu yangu ikakata chaji kabla hajamaliza kuongea na wewe. Hii hapa iangalie kama inachaji.
Baada ya hapo nikafanikiwa kubadilisha tairi, nikakimbia kuja nyumbani na nikapokelewa na wewe ukifanya mapenzi na mwanaume mwingine nyumbani kwetu!!
Mume akageuka na akaondoka na kubamiza mlango akatokomea nje. Unafikiri akirudi atachukua maamuzi gani?
Ungefanya nini kama ingetokea wewe ni mke au mume kwenye kisa hiki?

Nakutakia Ijumaa Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz