USIYALEWESHE MAHUSIANO YAKO kama mlevi wa pombe alewapo kupoza stress๐Ÿ˜Ž - EDUSPORTSTZ

Latest

USIYALEWESHE MAHUSIANO YAKO kama mlevi wa pombe alewapo kupoza stress๐Ÿ˜Ž

Image may contain: 2 people, people sitting, outdoor and nature
Kama ilivyo NGUMU KUTATUA MATATIZO KWA KUNYWA POMBE ndivyo ilivyo ngumu mno kwa;
Mtu kutafuta mbadala wa Mtu kwenye MAPENZI ili kupunguza ama kufubaisha matatizo ambayo yapo kwenye UHUSIANO WAKEโ„น
Ni kweli kabisa Kuna stress kwenye MAHUSIANO na Kuna muda mtu unaweza kujikuta unakata tamaa ya kuendelea BETTER ku-stop๐Ÿšซ kuliko kuendelea huku ukijua kabisa UHUSIANO WAKO USHAINGIWA SHUBIRI๐Ÿ˜ญ
Kinachotufanya kuyalilia MAHUSIANO ni ule urafiki ambao upo kwenye MAPENZI na huo ndo husababisha AMANI pamoja na FURAHA lakini kama unaona mienendo ya UHUSIANO/NDOA yako hauleti ile maana halisi ya mtazamo wako KUMBE UNA CHEAT ILI KUFAIDI NINI๐Ÿ‘‚
Huwezi ku cheat ili umbadiri Mtu kwamba aendane na ulivyokuwa unatarajia zaidi unajiongezea MATATIZO TU.
Huo ndo ulevi mbaya kuliko hata ulevi wa pombe๐Ÿป Maana mlevi wa pombe akinywa pombe husahau matatizo yake na pombe ukiisha matatizo yapo pale pale ila ujue USIKU ALILALA๐Ÿ˜…
Lakini ulevi wa MAHUSIANO huo hauna mbadala zaidi ya MARIDHIANO AU KUACHANA kwa sababu tabia ya Mtu ni kama ngozi, Kwamba Mtu anaweza kusema HATORUDIA ikawa kweli kama alikosea kwa bahati mbaya, ila kama Makosa yake hujirudia na neno SAMAHANI likawa kama nguzo ya wewe kumsamehe MY FRIEND kuiona nafuu ya UHUSIANO wako kwa Mtu wa aina hiyo ni sawa na kungojea MIMBA KWA MGUMBA
Ndo maana nikasema;
"USIYALEWESHE MAHUSIANO YAKO"
Kama umejaribu kuweka Sawa penzi lenu na huoni mabadiliko zaidi unaumia kila siku njia sio wewe kutafuta mbadala eti uwe na Mtu mwingine huku na anaekusumbua yupo HUO NDO ULEVI MBAYA๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
Kumbuka huyu mpya atajua unae MUME unategemea atakupa PENDO LA DHATI?
Anakupaje pendo la dhati na wewe unae mwingine? Maana yake atakulaghai ili muwe kwenye UHUSIANO pengine nae anazo sababu zake kuingia penzi lako na kwa upande wako akakudatisha huogopi kujikuta NJIA PANDA?
Usijaribu kuyalewesha MAHUSIANO yako kamwe hutakaa ufurahie zaidi utakuwa MHANGA WA MAPENZI kwa watu wawili wala usimuone ambaye ndiye anae takiwa kuwa nawe, Kila mmoja kwa nafasi yake UTAOGOPA KUMUACHA je nini maana ya kulewesha UHUSIANO wako?
MICHEPUKO SIO DEAL๐Ÿ‘ Ukiona huwezi kuendelea VUNJA UHUSIANO na kama unaona unaweza BAKI NJIA KUU๐Ÿ™‹
Kumiliki watu wawili ni HATARI KWAKO LAKINI PIA NI HATARI KWAO mwisho wako ni mbaya tu, Huna sababu ya MSINGI kuishi kwenye MAHUSIANO YA AINA HIYO Bora kukosa MAHUSIANO ili ukabaki salama, Kuishi kwingi Kuna starehe yake bwana weeee๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ๐Ÿ‘…
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria๐Ÿ˜Ž
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz