SOMA KISA HIKI KWA MAKINI......! - EDUSPORTSTZ

Latest

SOMA KISA HIKI KWA MAKINI......!

Couple having argument on the couch at home in the living room Stock Photo - 42399621

Baba mmoja alikua amekaa uani katika nyumba yao mpya ambayo walikua wamejenga na mkewe. Baada ya ndoa ya miaka 20, baada ya kuteseka miaka 20 katika nyumba ya kupanga hatimaye wlaifanikiwa kujenga nyumba yao nzuri.
Nyumba yao ilikua kubwa na walikua wakitumia upande mmoja na upande mwingine wa mabanda ya uani waliweka wapangaji, Yule Baba akiwa amekaa mke wa mpangaji mmoja alipita mbele yake kuteka maji.
Kama unavyojua macho hayana pazia, Baba yule alishindwa kujizuia kuangalia makalio makubwa ya yule binti mchanga kab9is aambaye alikua hata hajajalaiw akupata mtoto. Mwili wake ulikua umeumbika na aliuangalia kwa matamanio, wakati akifanya hivyo hakujua kuwa mkewe aliku anamuangalia na alipogeuka alimuona mkewe akirudi ndani na hasira zake huku akiw amenyongonyea.
Yule Baba alirudi ndani kumuangalia mkewe ambaye alilazimisha tabasamu kana kwmaba hakuna kitu kimetokea, alijaribu kumuuliza mbona vile mkewe akasema hapana hamna shida. Siku ile iliisha kimyakimya, lakini mkewe hakuw ana raha na hata kesho yake mkewe alikua mtu wa wasiwasi sana. Siku hiyo usiku baada ya chakula, wakiwa chumbanai Mama akitaka kuzima taa Baba alimuambia acha kuna kitu nataka kukuonyesha.
Alimuita mkewe na kumuambia akae karibu yake kitandani, kisha alichukua albam ya picha iliyokua mezani na kuanz akuifungua. Alianza kumuonyesha mkewe picha zao za utotoni na nyingi za harusi, walianz akuongea na kukumbuka matukio yote ya harusi yao. Lakini pia alimuonyesha picha za siku nyingi walizopiga katika matukio muhimu, “Unakumbuka hapa mke wnagu, nilikua naumwa nikalazwa wiki mbili, nilikoda sana na ulikua unanilazimisha kula chakula kama mtoto mdogo.
Nakumbuka mume wangu, hapa ndipo nilitoka kujifungua na tumbo langu kubw anilikua nalichukia ukaw aunalibusu kila siku kusema nimependeza. Hapa mke wangu nilisimamishwa kazi nikawa natoka tu nadanganya naend akazini kumbe nazunguka sokoni kubeba mizigo. Mume wangu hapa ni kipindi kile mtoto wetu aliugua mpaka kukaribia kufa, unakumbuka yule Bibi ambaye alitusaidia kumpa dawa sijui hata yuko wapi inabidi tuende kumsalimia tumpelekee hata zawadi”
Walimaliza kuangalia picha kisha kuanza kukumbushana matukio ya zamani. Tumetoka mbali mume wnagu unakumbuka wakati tunajenga hapa tulivyoanza kw shida.. nakumbuka mke wnagu tulilazimika kubeba maji wenyewe. Yaani nilijifunza hata kufyatua matufali, unakumbuka kipindi kile…unakumbuka kipindi kile… walikumbushana sana mambo waliyopitia na mwisho yule Baba alimuambia mkewe.
Najua huna amani, umeniona namuangalia yule B8inti nikwlei nilifanya vibaya lakini hata sikumtamani kwani hata nikimpata leo nitaupata mwili lakini sitayapata maisha, kwako mke wangu kuna vingi vya kupenda kuliko hata mwili. Mke wangu mke wa jirani nisawa na nyumba ya jirani, unaweza kuiona nzuri na kuitamani lakini mwisho wa siku itakukinga mvua tu wakati ukipita lakini kamwe haiwezi kuwa yako.
Nakupenda kwasbabau miaka 20 iliyopita ulikua binti na mimi nilikua kijana, sasa wewe ni mama na mimi ni Baba. Kwa macho ya wengine tumezeeka lakini wewe kwangu ni kijana kwani naona kitu kile kile nilichokiona miaka 20 iliyopita nilipoamua kukuoa. Wewe ni nyumba yangu hata kama inanyufa ni za kwnagu, najua hutaishia tu kunikinga kw a mvua bali pia utanipa usingizi na amani. Huna haja ya kuona wivu na kama yule mpangaji anakunyima amani basi niambie kesho anaondoka.
Mkewe alimuangalia mumewe na machozi yalianza kumtoka, walikua wametoka mbali sana alimuambia. Hapana haninyimi amani kama ulivyosema wewe pia ni nyumba yangu, sitaki niruhusu uzuri wa nyumba za majirani uninyime usingizi. FUNZO; kuna watu wengi wapya watakuja katika maisha yako, utawatamani na mwenza wako ataona wivu, ni kazi yako kumkumbusha kila siku kwanini unampenda na kwnaini yeye ni bora zaidi.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz