*🍇MHESHIMU MUME WAKO.🍇* - EDUSPORTSTZ

Latest

*🍇MHESHIMU MUME WAKO.🍇*

Portrait Of Loving African American Couple In Countryside Stock Photo - 31066702
Hakuna kitu ambacho kila mwanaume anapenda akipate kwa Mke wake kama KUHESHIMIWA.🍇
Tukumbuke kua silka ya mwanaume na uasili wake na maumbile yake ni kuheshimiwa na mwanamke ,sababu mamlaka haya amepewa na Allah.🍇
Bora ahisi kua humpendi anaweza kuvumilia,kuliko kuona kua humheshimu sababu hio ni asili yake hawezi kukubali kuipoteza.🍇
Asilimia kubwa ya wanawake tuna tabia ya dharau ,kiburi ,jeuri ,maneno ovyo na tunasahau kua hata tukafanya ibada ya aina gani bila ya kumheshimu na kumtii Mume hatuna tutachovuna.🍇
Allah hakuwahi kuchagua Mtume mwanamke,haturuhusiwi kuwa makhalifa katika ardhi,hatutakiwi kuozesha wala kutoa idhini ,wala hatutakiwi kukaa hata uimamu. Hii ni kuonesha kuwa tunatakiwa tuwe chini ya miguu yao sio juu ya vichwa vyao.🍇
Ni wajibu wako kumheshimu na kumtii Mume wako kwa asilimia zote, hata kama una hela na unamlisha na kumvisha bado haiwezi kupunguza heshima yake ,atabaki kuwa msimamizi na madaraka yake yako pale pale.🍇
Heshima yako kwake itajenga ndoa imara yenye mapenzi zaidi, na italeta furaha na neema kwenye ndoa yenu na mtaepuka mizozo na mikwaruzano ya Mara kwa Mara.🍇
*🍇Alieyapenda ayachukue🍇*
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz