NASEMA NA WEWE MWANAMKE; - EDUSPORTSTZ

Latest

NASEMA NA WEWE MWANAMKE;


Usitafute UPENDO kwa Mwanaume Kwani ni wajibu wake KUKUPENDA.
Ila ukiona hakuna UPENDO juu yako na upo nae ujue kwamba kuna anayependwa, Msijidanganye kwamba wanaume hawana UPENDO bali Jiulize Kwanini HAKUPENDI WEWE?
 KUHUDUMIWA ni wajibu wa Mwanaume.
 MATUNZO ni wajibu wa Mwanaume.
 KUKULINDA ni wajibu wa Mwanaume.
 HAKI YA TENDO LA NDOA wajibu wa Mwanaume.
Wala usijitaabishe kulazimisha hayo, Kwani ndiyo sehemu ya uhalisia wa MUME lakini ikiwa ili uyapate hayo ni mpaka UPIGE KELELE rafiki unakula upepo hapo.
Wanawake mnajidanganya katika MABADILIKO kwamba unayoyaona leo ni changamoto, Na yatakayokuja baadaye mnayatarajia pengine hiyo ni IMANI lakini kwenye ISSUE ya MAPENZI hatuna sababu ya kutarajia Kwani hilo sio FUMBO LA MUNGU.
Mapenzi ni UTASHI wa ki bin adam, kukubari ama kukataa ni uwezo wa akili na Moyo, Kwanini HAKUNA MWANZO MBAYA KWENYE MAPENZI? Siku zote Mwanzo unakuwa mzuri kwani kila mmoja na shauku ya HITAJI LAKE KUTIMIA ila siku zinavyokwenda ikiwa wawili waliingia kwa sababu zao PENZI LINAKWENDA MLAMA🏊.
Ishi kwa uhalisia wako na ukubaliane na uhalisia uliopo ili akija Mwanaume akaonyesha KUKUPENDA mshike huyo, Maana ni nadra sana kukuta Mwanaume ametoa PACKAGE YAKE YA UPENDO ila ni rahisi kwa aliyeandikwa kwa moyo wake.
Wanawake wengi MNAOLEWA na wanaume wa watu, Yaani badala ya KUOLEWA na mwanaume wako kwa sababu ya muda kuyoyoma unajitwalia MUME WA MWINGINE rafiki itabaki historia kwamba ULIOLEWA ila kwa uhalisia utakuwa UNAISHI NA MUME WA MTU kutwa anatanga kumtafuta wa kwake na wewe unabaki ukilalama kama ndama wa mbuzi🐐.
 MUME wako hawezi kukuacha ukilia.
 MUME wako hawezi kukudharau.
 MUME wako hawezi kukuwekea mipaka.
 MUME wako hawezi kukupa UPWEKE.
 MUME wako hawezi kukusaliti.
 MUME wako hatajaribu kukuacha PEKE yako.
 MUME wako hawezi kukulinganisha na kazi zake.
Na mengine yanayofanana na hayo, Sasa wewe endelea kungojea NDOA IREJEE KWENYE MISINGI YAKE huku aliyekuoa sio MUME wako ila haraka zako ukaparamia MUME wa watu, Kumbuka mkewe YUPO ANAMNGOJEA muda ukifika ndipo utabaini MBIVU NA MBICHI.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz