MKE AU MUME ANAPOKUWA WAMEINGIZA REHANI NDOA YAO KWA TOFAUTI ZA KI MAPENZI NJIA SAHIHI NI KUTATUA HUU MGOGORO NI HII! - EDUSPORTSTZ

Latest

MKE AU MUME ANAPOKUWA WAMEINGIZA REHANI NDOA YAO KWA TOFAUTI ZA KI MAPENZI NJIA SAHIHI NI KUTATUA HUU MGOGORO NI HII!

Image may contain: 2 people, people sitting and indoor
MARIDHIANO
Lakini ndoa nyingi zimeghubikwa na sintofahamu juu ya UHUSIANO baada ya kila mmoja kuamua kutafuta NAFUU ya mapito anayopitia kwenye NDOA yao, Wengi wao wanafikiria kutafuta NAMNA YA KUJINUSURU NA STRESS ZA NDOA
Wengi wameingia kwenye NDOA bila kujitathimini mwisho wao ukawa mbaya na uliojawa na UPWEKE kwa sababu NDOA HIYO HAIJALETA MAANA YA NDOA.
Mwanaume anahangaika kujazia PACKAGE ya ndoa yake kwa kuwa na MCHEPUKO kama sio MICHEPUKO😎
Mwanamke vivyo hivyo nae anahangaika kuitafuta PACKAGE YA UPENDO ALOKUWA ANADHANIA MUMEWE ANAO kwa kuwa na MCHEPUKO huko nje💃
Mwisho wa yote ni wawili hao kukutana NYUMBANI KWAO "KWENYE FAMILIA YAO" huku kila mmoja akiwa na PUMZIKO LA MAJUTO YA KWANINI NILIOLEWA💑/NILIOA💑
Michepuko ni kama dawa ya kuchua mahala ambapo Mtu anahisi MISURI haijakaa sawa😂😂
NAJIULIZA
JIULIZE
Tayari ushaona NDOA haikwenda kama ulivyoitarajia KWANINI USIKUBARI MATOKEO ama uendelee hivyo hivyo au usiendelee ili kuepuka kupoteza MUDA wako pamoja na HAIBA YAKO?
Kwa sababu ukiendelea unakuwa umeamua na ikiwa utaacha utakuwa umeamua, Kwa maana fupi yote yako ndani ya uwezo wako KUAMUA kipi kinafaa kuwa kipaumbele chako katika MAHANGAIKO YA NDOA YAKO.
Nijuavyo Mimi KUCHEPUKA sio suruhisho la KUIPONYA NAFSI YAKO bali unakuwa kwenye kuupoza MWILI ili japo usiumie kwa kila kitu, Pengine tatizo la NDOA yako ni juu ya TENDO LA NDOA lakini je umezungumza na mwenza wako hata ukajua kwamba hawezi kuwa sababu ya uhitaji wako?
Je ni TABIA halisi ambayo anayo mwenza wako na huipendi UMEZUNGUMZA NAE?
Kama ni NDIYO na ukajiridhisha kwamba hakuna suruhu kuepuka adha uipatayo JE WAZAZI PANDE ZOTE MBILI WANAJUA TATIZO HILO LINATESA NDOA YENU?
Kama ni NDIYO na hapakuwa na UPONYAJI WA NDOA YENU naomba nikwambie HERI NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI.
Yaani bora ukaachana na NDOA hiyo kuliko KUCHEPUKA Kwani KUCHEPUKA kuna madhara mengi ila ninalo moja tu ambalo litakufanya ukose FURAHA MAISHANI MWAKO;
Kudhania MCHEPUKO ni suruhu ya tatizo linaloikabili NDOA yenu wakati huwezi KUCHEPUKA ukalikwepa tatizo la NDOA yenu kwa maana moja tu;
"BAADA YA KUCHEPUKA UKAKIDHI HAJA ZAKO STILL UTARUDI KWENYE NDOA HIYO"
Huo ni ujinga wa kiwango cha PHD😂😂
Bora KUBWAGA MANYANGA CHINI UKASEPA NA 50 ZAKO pengine utakutana na MJINGA MWENZIO Kwani wengi tunapokuwa kwenye NDOA kutokana na UPENDO tunageuzwa kuwa WAJINGA💆
Maana kati ya wana NDOA ambaye huteseka na NDOA ni Mwanamke kwa sababu yeye huwaza zaidi namna ya kujikomboa Kwani yeye ALIOLEWA😭😭
ANGALIZO;
Mwanamke usijaribu kuruhusu MWILI NA AKILI YAKO IKAMILIKIWA NA WANAUME WAWILI maana yake HIWEZI KUKWEPA MTIHANI HUO🚫
Ni Sawa na Bin adam kula nyama ya Bin adam wallah HUWEZI KUACHA😅😅😅
Ukiona jamaa anazingua tafuta namna ujikomboe kuliko kusaliti maana NDOA itakuwa na nafasi yake kwako lakini pia MCHEPUKO utatawala AKILI YAKO mwisho wako mbaya niamini nakwambia, Mwanaume hata akichepuka eti wanamwita KIDUME kumbe nao ni UKOSEFU WA UTULIVU WA MIHEMKO YAKE TU😅😅




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz