Mitihani ya MAPENZI ni kama ukikutana na mtu na MOYO wako ukapiga, mikono ikatetemeka na magoti yako yakakosa nguvu HUYO SIE.. - EDUSPORTSTZ

Latest

Mitihani ya MAPENZI ni kama ukikutana na mtu na MOYO wako ukapiga, mikono ikatetemeka na magoti yako yakakosa nguvu HUYO SIE..

Image may contain: 2 people, people sitting and outdoor

Mitihani ya MAPENZI ni kama ukikutana na mtu na MOYO wako ukapiga, mikono ikatetemeka na magoti yako yakakosa nguvu HUYO SIE... Kama ukikutana na MWENZA wa nafsi yako UTAJIHISI KUTULIA! Maana huyo ndiye ambaye anautuliza moyo wako, wala huwezi kupata wasiwasi wala hakuna ubishi huyo ndiye, Upendo sio HISIA bali Upendo ni KITENDO, lakini pia Upendo ni JUKUMU... Penzi la kweli linahusisha kujitoa na zoezi la upeo ki akili,Upendo kama nia ya kujikuza binafsi kwa lengo la kujipanua wewe au mwingine kukua kiroho! Upendo wa kweli ni tendo la nia ambalo linazalisha HISIA za ndani za upendo au mapenzi ya ziada, ni sahihi kusema UPENDO ni kufanya UPENDO ili kumsogeza Mwenza wako akukaribie ki MAHABA... Na hapo ndipo utayataja MAPENZI KUWA UPENDO WENYE HISIA.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz