MAUMIVU YA MAPENZI DAH WE ACHA TU - EDUSPORTSTZ

Latest

MAUMIVU YA MAPENZI DAH WE ACHA TU

Image result for MAPENZI YA MBALI; HATAKI UENDE KWAKE ANATAKA AJE YEYE KUKUTEMBELEA.
#inasikitisha

1)Unaweza kuta mtu amekonda afya mbovu, ukafikiri labda ana virusi vya ukimwi ukaanza kumpa ushauri nasaha na kumshauri akapime ili ajijue na kuanza dozi ya ARV mapema kumbe mwenzio anaugulia MAUMIVU YA MAPENZI.

2) unaeza shangaa mtu kajiua, kanywa sumu au kajinyonga ukafikiri ni stress za maisha, madeni au kauawa kumbe chanzo ni kuumizwa na MAUMIVU YA MAPENZI kashindwa kuvumilia kaamua kujiua.

3. Unaeza kutana na mtu kachanganyikiwa njiani anaongea mwenyewe kama tahira au kichaa ukajua karogwa kumbe chanzo ni MAUMIVU YA MAPENZI kaumizwa na mtu ambaye hakutarajia haamini maana walipendana mno.

4. Waeza shangaa dereva anapindua gari kizembe ukafikiri labda alilewa kumbe alikua anaugulia MAUMIVU YA MAPENZI kashindwa kuvumilia mawazo yamemtawala hajielewi mzimu wa aliyemtenda umeitawala akili yake anaona barabara imepinda kumbe imenyooka mwishowe anatumbukiza gari mtaroni.

5. Waeza shangaa jamaa anauza nyumba, gari, kiwanja, vitu vya ndani n. k na kutumia fedha zake zote kunywa pombe kulewa na kulala baa ukafikiri labda kachanganyikiwa kumbe anaugulia MAUMIVU YA MAPENZI akili yake inamtuma kuwa pombe pekee ndio yaeza mpooza na machungu ya kutendwa.

6. Waeza kutana na rafiki au ndugu yako ukamsalimia asikuitike, asitake kukujua wala kukuamini ukafikiri ameharibika tabia amekua na midharau su kiburi kumbe la hasha anaugulia MAUMIVU YA MAPENZI hamuamini mtu yeyote tena chini ya jua kila akimkumbuka aliyemtenda anaona wanaume/Wanawake wote mbwa tu.

7. Unaeza kuta njemba kubwa ya miraba minne iliyojazia misuli kama Anorld Schwarzneggar inalia kama mtoto mdogo ukatafakari ukahisi kutokana na nguvu zake hakuna mtu anayeweza kuiliza labda itakua imefiwa na mzazi hahahahahaaaaaa duh kumbe njemba nayo inaugulia MAUMIVU YA MAPENZI imetendwa.

Aisee bado natafakari nini siri iliyojificha ndani ya MAPENZI maana kiukweli inapotokea watu wamependana kiukweli alafu wakabwagana ghafla inakua MAUMIVU MAKALI zaidi ya msiba.

2020 ukawe mwaka wa amani na furaha moyoni mwako Mungu akuepushie MAUMIVU YA MAPENZI uhusiano au ndoa yako ikawe ya furaha, upendo, uaminifu na baraka tele.

Niambie ni point ipi hapo juu imekugusa zaidi kisha SHARE post hii.

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz