MAMBO MATANO AMBAYO HUTAKIWI KUMUAMBIA MUME/MPENZI WAKO! - EDUSPORTSTZ

Latest

MAMBO MATANO AMBAYO HUTAKIWI KUMUAMBIA MUME/MPENZI WAKO!


Katika mahusiano au ndoa mara nyingi wanawake hupenda kuongea, mara nyingi hujikuta katika mitego flani ambapo wao huamini kwa kuwa wawazi labda ndiyo wataonekana kama wanapenda, si waongo na wataaminika zaidi. Hapana, katika mapenzi ni lazima mambo mengine ubaki nayo na upambane na hali yako, haya ni mambo matano ambayo wewe mwanamke hutakiwi kumuambia mpenzi/mume wako.
(1) Acha Kumuambia Tabia Mbaya Za Mama Yake; Mama yake ana kidomo domo, anatabia mbayambaya, labda anachepuka, ni mbea wa kusutwa na tabia nyingine mbayambaya, labda anafahamu na anakuulizia jifanye hujui? Lakini hajui, acha kujitia kimbelembele cha kumuambia kuhusu tabia mbaya za Mama yake, kumbuka yule ni Mama yake. Hataki kuzisikia na wala hapaswi kuambiwa hasa na wewe.
Mama ndiyo kiumbe pekee anayempenda labda ukiacha wanae, ingawa anaweza kuwa anazijua lakini akijua na wewe unazijua na zinakuchukiza ataumia zaidi. Hakuna kitu ambacho kinamchukiza mwanaume kama kuambiwa mabaya ya Mama yake, hivyo acha kumuambia. Hapa sizungumzii kama Mama yake anakunyanyasa, hapana nazungumzia tabia mbayambaya za Mama yake ambazoo hata hazikuhusu.
(2) Acha kumuambia kuwa rafiki zake wanakutaka; Kuna rafiki yake mmoja kila wkati mkikutana naakuangalia kama anataka kukutongoza, napengine labda ashakutongoza kimtindo. Hembu kataa kivyako kama mtu mzima na nyamaza, acha kumuambia kuwa rafiki yake anakutaka, jifuneze kukata akivyako, utakapomuambia mbali ya kuumia lakini atakua na wasiwasi, atakumbuka ukaribu wote amabo ulishawahi kuwa naye.
Atawaza labda ushafanya mambo naunajihami, lakini atawaza ni wangapi wankautongoza husemi, hatakuamini tena. Muambie kama unaona labda kaziadisha na anataka kukudhuru ila kama ni tongoza ya kawaida pambana kivyako, kumbuka anaweza asijali kuhusu tabia ya rafiki yake lakini akajali wewe akiwaza hivi wakati unatongozwa ulimtegaje.
Nyamaza na kama akijua basi muambie kweli alikua anaongeaongea ujinga ukamziba mdomo na onyesha ulichukulia kama utani tu na mambo ya kipuuzi hukutilia maanani. Usionyeshe kana kwmaba labda ulichukualia siriasi, onyesha kama kilikua ni kitu cha kipuuzi na hukuona haja ya kumuambia upuuzi huo, ila sio kila unapotongozwa hata kama si rafiki yake unasema, ni ujinga jiamini na jifunze kukataa kivyako.
(3) Kamwe usimuambie kuwa ulishawahi kumsaliti X wako; Kuna watu wakianzisha mahusiano wanafunguka kila kitu, kwmaba ulishakua katika mahusiano unaanza kufunguka sababu za kuachana na X wako, eti ulimsaliti, hapana usimdanganye na kama hajui basi muambie mlishindwana tabia basi, labda kama tukio lako la kufumaniwa lilikua kubwa likajulikana kila mahali ila kama ni ile ya kimyakimya kufa nalo ukimuambia hatakuja kukuamini atajua ni tabia tako na yeye unaweza kumfanyia hivyo.
(4) Usijekumuambia kuwa ulishwahi kutembea na mume wa mtu; Ndiyo hiki ni kitu kingine ambacho kitamfanya asikuamini, anajua yeye si wakwanza lakini huna haja ya kutaja ulitembea na nani, acha kutangaza kuwa ulitembea na mume wa mtu, hatakuja kukuamini kwani kwa wanaume wengi hiki ni kiwnagoc ha juu cha umalaya na ataona kuwa wewe huheshimu taasisi ya ndoa.
Ajue huko kivyake basi, lakini kama akijua ulikua unatembea na mume wa mtu kusema kweli hatakuheshimu na ni ngumu kukuamini kwani anajua kuwa wewe umekaa kimaslahi na anaamini kuwa kama uliona poa kutembea na mume wa mtu basi hata wewe ukiwa mke wa mtu hutaona shida kutembea na mwanaume mwingine. Hivyo dada yangu acha kuzungumiza sana mahusiano ya nyuma na kama kuna mume wa mtu usimtaje kabisa.
(5) Acha kumuambia tabia mbaya za marafiki zako; Ndege wafananao huruka pamoja, kama kila siku unamuambia tabia mbaya kuhusu marafiki zako halafu bado unawaita marafiki basi jua kukuamini iytakua ngumu. Rafiki yako ni Malaya anatembea na mume wa mtu hujali na kila siku unamzungumia, hata kama unazungumza kwa namna ya kile kitu kukukera lakini ilimradi unamkubali kama rafiki absi umekubali na tabia zake.
Muache ajue huko lakini si kwa wewe, najua kuna wakati unatamani kumfanya mume au mepzni wako kama shoga yako na kwakua unamuamini na umepewa umbea wa moto unataka kumuambia. Umuambie anavyochuna, anavyohongwa, anavyofanya mapenzi kinyume na maumbile na ujinga mwingine mwingi. Hapana, unapomuambia mume au mpenzi tabia mbaya za marafiki zako ni kama unamuambia tabia zako, ataamini na wewe unafanya hatakama hufanyi.
Mwisho nimalizie kwa kusema kuwa, mfanye mume wako rafiki lakini katika urafiki huo kua makini unapoongea usiwe comfortable sana kwani kumbuka kuwa yeye mbali ya kuwa rafiki lakini ni mumeo. Kuna mambo yanafa akumuambia rafiki lakini yakamuumiza mume hivyo hembu kuwa makini, kila unapofungua mdomo unatakiwa uwaze kama kitu unachokiongea kina umuhimu na kina faid aya kuongewa?
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz