HUTONGOZWI KWASABABU KILA WAKATI UNA USO WA KAZI: - EDUSPORTSTZ

Latest

HUTONGOZWI KWASABABU KILA WAKATI UNA USO WA KAZI:

Mwanamke ambaye kila saa anajifanya yuko siriasi na kila wakati ana uso wa huzuni ni mwanamke mgumu sana kutongoza na binafsi nikikusalimia mara moja nikaona ‘uso wa mbuzi, kauzu’ naendelea na maisha yangu. Kuna watu ukikutana nao kila saa wamekasirika, wengine unaweza kufikiri labda wameambiwa kila salamu inatia mimba, unamuambia za saa hizi umependeza utasikia “Halafu wewe Kaka tabia zako nazijua… mimi nina mtu wangu… nataka mtu siriasi…”
Mmekaa sehemu na washikaji mnaongea mnataniana kimeongelewa kitu cha kipuuzi ili mcheke yeye utasikia “Acheni hayo mambo yenu…si mkue…kueni siriasi…” kwakifupi kila wakati yuko siriasi, ukimuangalia usoni eidha ana huzuni au kakasirika kana kwamba amebeba matatizo ya dunia. Hata kama una matatizo kiasi gani, hembu yaache nyumbani na tabasamu.
Hakuna mwanaume atakutongoza kama kila akikuangalia tayari umenuna, atawaza yeye ana matatizo yake sasa kwanini akufuate wewe wakati una matatizo. Unakasirika vitu vya ajabu ajabu, kitu kiliongelewa kwaajili ya kuchekwa wewe una nuna na unadhani watu wanakuongelea wewe. Hapo kwanza mtu akikuona tu atakukimbia lakini kutakua na kasifa mtaani kila mtu akitaka kukutongoza utasikia “Yule hamtawezena ana kisirani sana utachanganyikiwa, tafuta mwingine!”
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz