KWANINI USIINGIE KWENYE PENZI LA MHANGA WA PENZI⛔ - EDUSPORTSTZ

Latest

KWANINI USIINGIE KWENYE PENZI LA MHANGA WA PENZI⛔

Image may contain: 1 person, sitting and indoor
Kwanza nikiri kwamba KUUJUWA UKWELI WA MTU NI NGUMU kutokana na ukweli kwamba MOYO wa mtu ni PANGO LENYE KIZA KINENE... Mtu anaweza kuwa na tabasamu lakini moyo wake umejaa machungu, Kuingia kwenye mahusiano na mtu ambaye AMA ANATOKEA KWENYE PENZI AU NDOA ALOIPENDA NA AKATOKA KUTOKANA NA KUKOSA FURAHA NA AMANI ni jambo gumu na kwa hakika kumuweka sawa mtu huyo ni mtihani ambao kufauru unahitaji rehema ya MUNGU🙏
Aliimba DIAMOND🎹 "MCHANA NAEZEKA JIONI WATU WANAKUJA KUBOMOA"
Kwamba ukiwa na mtu ambaye ametoka kwenye mahusiano anayoyapenda ila kuna mambo yamemfanya atoke huko maana yake wewe UTAKUWA KAMA PANADOL KWENYE MAUMIVU YA JINO huponyeshi ila unapoza😂😂😂
Maana mpaka dakika hiyo mwenzio anawaza alikotoka na wewe unapambana kumuweka sawa, unaweza kufarijika na majibu mazuri toka kwake JE MOYONI UNAJUA ANAWAZA NINI?
Ni kweli kabisa HAKUNA MTU ANAINGIA MAHUSIANO BILA KUWA ANATOKEA KWENYE MAHUSIANO ila kuna watu wanakuwa wamejeruhiwa watokako na anapokuja kwako ANATAKA FARAJA TU ili avuke salama kwenye mapito amepitishwa na mwenza wake huko atokako, Penzi lolote linaweza kuwa gumu mwanzoni but MAZOEA yakasababisha Mtu akakupenda sana, Shida ni moja tu;
"UPENDO HAUJIFUNZI ILA NI NATURE"
Mtu akikupenda kwa kujilazimisha iko siku atajilazimisha kukuacha😂
Niamini nakwambia MAPENZI mazuri ni yale ambayo tangu siku ya kwanza yaliongozwa kwa NATURE "uhalisia" kwamba ulipomuona uliingiwa kitu ndani yako, Alipokuona aliingiwa kitu ndani yake, Nafsi inatabia ya kuongea na kama kweli mtu anakuwazia lazima nawe utajikuta unamuwaza na kuna wakati mkapishanisha msg📩 ama simu📲
Na hapo ndipo utajua kwamba NAFSI ZINA WASILIANA KWA SABABU YA UPENDO WA DHATI
Unaweza kumpokea mtu usijue anakupa nafasi akiwa na mtazamo gani ila nataka nikwambie KABLA HUJAJIWEKA MZIMA MZIMA KWA MTU JARIBU KUJUWA ANAKOTOKA KUNA MTAZAMO WA WAMEACHANA AMA HASIRA ZINAWATENGA KWA MUDA🤷🏽‍♂
Kataa kuwa daraja la MATESO YA MTU bali itafute sababu ya wewe kuwa na Mtu ambaye yeye mwenyewe anajua bila wewe NAFSI YAKE HAIJAKAMILIKA💃💃
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz