MAISHA YA MWANA MKE YANAHITAJI HURUMA YA MWANA MUME! - EDUSPORTSTZ

Latest

MAISHA YA MWANA MKE YANAHITAJI HURUMA YA MWANA MUME!

Image may contain: 2 people, people sitting and indoor
Kila Mtoto wakike kwenye maisha yake anahitaji KUTHAMINIWA💃
Mwana Mume atakaye ijua THAMANI YA MWANA MKE kwa hakika atakuwa ameuponya moyo wake🤦🏻‍♀
Ki maumbile Mwana Mke ni mpweke ndo maana Mtoto wakike anapokuwa amevunja ungo hutamani maisha ya NDOA na sio kuwa na Mwanaume, Mwana Mke anapokuwa ameingia mahusiano ama kuolewa na Mwanaume ambaye anakuwa BABA KWAKE kwa hakika hujiona ni BINTI, MSICHANA, MWANAMKE lakini pia hujiona kuwa yeye ni special kwenye ULIMWENGU huu, Kwani Maana halisi ya BABA ni Mwanaume ajuaye wajibu wake kwa Mwanae👌
Ndo maana kesi nyingi kwenye MAHUSIANO/NDOA ni Mwanamke kukosa UPENDO wa BABA! Kwamba Wanaume wengi wanaingia kwenye Mahusiano/Ndoa kwa kumtazama Mwanamke kama mvuvi kukosa samaki lakini kitoweo lazima apeleke nyumbani🤣
Mwanaume anapokuwa ameshindwa kujuwa THAMANI YA MWANAMKE maana yake Mwanamke huyo atakuwa amempata Mwanaume ambaye anabaki kuwa Mwanaume badala ya kuwa BABA kwa Mwanamke wake🙆🏿‍♂
Mwanamke anapokuwa amempata Mwanaume akawa MUME maana yake atatajwa kama BABA... Ndo maana wanawake wengi wamekuwa kwenye NDOA lakini hawajui MAANA YA NDOA baada ya waume zao kusimamia mfumo DUME😭
Wakati huo huo Mwanaume anataka Mwanamke ahudumie familia😇
Kuna wakati nasema wanawake nanyi mmekuwa wavivu wa kufikiri, Yaani Mtu anajidai kwamba ni MUME wako na hajishughurishi kuhudumia familia n then nawe umeganda kama BARAFU kwenye jokofu ukijipa misifa kwamba UMEOLEWA🤷🏽‍♂
Milembe panakuhusu nenda japo upime akili🤣
Mwanamke anapokubari kuwa mdhaifu kwa Mwanaume ambaye sio MUME kwa uhalisia huyo ni Sawa na NZI KUFIA KWENYE KIDONDA😂😂
Yaani si bora usiwe na ndoa lakini uko na FURAHA YA NAFSI? Kutwa kulalamika juu ya Mwanaume wako lakini Bado upo tu TENA BORA JAMAA AKUKOMESHE KABISA MAANA HUJITAMBUI!
Maisha ni FURAHA... Na FURAHA ni Maisha, Nani aje akupe FURAHA wakati wewe mwenyewe hujui Furaha yako inapatikanaje? Kama huwezi KUPAMBANIA unachokihitaji kaa kimya unatuumiza masikio👊🏿
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria🙋🏻‍♂
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz