"KILA PENZI LA DHATI LINA WIVU NDANI YAKE" - EDUSPORTSTZ

Latest

"KILA PENZI LA DHATI LINA WIVU NDANI YAKE"

Image result for mapenzi wakubwa

Kwa utafiti wangu nimechunguza na kubaini kwamba "KILA PENZI LA DHATI LINA WIVU NDANI YAKE" Maana halisi ya wivu ni "UBINAFSI" Ukiona Uko na Mtu kwenye MAHUSIANO/NDOA na hasikii UBINAFSI WA WEWE KUWA WAKE PEKE YAKE ujue kwamba yupo ambaye aliishawekwa kwenye "MOYO" na wewe ukaondolewa ukabakizwa kwenye akili pengine MNA WATOTO, MMEJENGA AMA KUMILIKI MALI KADHA WA KADHA... Na mengi ambayo yanamsababisha kuona kwamba uwepo wako ni kwa sababu fulani fulani, WIVU una matabaka makuu mawili;
KUTOCHANGIA PENZI NA MWINGINE.
KUTOMSIKIA MWINGINE.
Mtu anapokuwa hataki kuchangia penzi maana yake anao ubinafsi na amejipanga kulibeba penzi lake mwenyewe bila kuchangia na mwingine, Kuchangia haimaanishi ni KUSHIRIKI TENDO LA NDOA TU Kuna hatari mbaya wengi hawaijui Naomba niseme leo "MAWASILIANO NI CHANZO CHA UKARIBU KWENYE MAPENZI" Kama upo na Mtu na anakuimbia anakupenda lakini Kuna wakati unabaini anawasiliana na MWANAUME/WANAUME wengine nao wakipenyeza maneno ya kumbembeleza kwa vyovyote akili yake haiwezi kuwa na utulivu, NA KWANINI ARUHUSU HALI HIYO NA WAKATI TAYARI ANAKWAMBIA ANAKUPENDA NA MKO PAMOJA? Huyo ni mtu hatari kwa moyo wako usipomdhibiti UTAPATA SHIDA MBELE YA SAFARI YAKO.... Nakuja kwa Mtu ambaye yeye hataki kusikia Mtu mwingine akinyemelea penzi lake maana yake huyo amejipanga "KUFA NA KUPONA" kwa umasikini ama utajiri ila PENZI LAO LISONGE MBELE! Huu wivu ni mzuri na una DHAMANA kubwa kwenye moyo wa mtu huyo, WIVU huo ukikatiza mbele zake AMA ZAKO AMA ZAKE😂
Kuna wakati unaweza kuishi na mtu hata miaka miwili asikuonyeshe WIVU ni kwa sababu moja tu "UMEMJENGA KWENYE IMANI" lakini siku akija kuhisi Uko uongo mdogo umedanganya mara nyingi MOYO huugua na kuanza ku-imagine mambo mengi kiasi kwamba yapo ambayo hayatakuwa katika makosa yako lakini chanzo ni wewe kumjenga mwenzi wako kwenye IMANI na baadaye ukajikuta umekosea kitu kidogo sana, IMANI kubwa hubomolewa na dosari ndogo hasa inayohusu UAMINIFU... Mfano wake;
UMEMJENGA MWENZIO KWAMBA WEWE NI MWAMINIFU NA HUNA MWINGINE ZAIDI YAKE
HALAFU SIKU MOJA ANAONA UJUMBE WAKO UNAMUANDIKIA MTU MWINGINE "Ninakupenda"
Nisikufiche hakuna kitu ambacho hubomoa ukuta wa Mapenzi kama Mtu anapohisi kwamba anadanganywa yupo peke yake na kumbe Kuna mwingine, Inauma sana na labda nikwambie kwa ufupi sana "HATA AKIKUSAMEHE ITATOKANA NA NAMNA GANI ANAJARIBU KUUTETEA MOYO WAKE ILI ASIJE KUKUACHA BADO ANAKUPENDA BUT MWISHO WA YEYE KUKUPENDA NI SIKU ILE AMEONA UNAMUANDIKIA MWINGINE UNAMPENDA"
Nature ya neno NAKUPENDA linatajwa na kuleta maana kwa Mtu mmoja, Ukimpenda mzazi utaanza na "MAMA NAKUPENDA, BABA NAKUPENDA" Lakini ukiwa unamtajia mpenzi wako NAKUPENDA sio lazima utaje wadhifa ama jina lake, Kwa hiyo NAKUPENDA YA UPENDO WA KULETA IMPACT KWENYE MOYO WA MTU INATOKANA NA MAHUSIANO! Wivu husitawi kwa sintofahamu kuzidi kushika kasi, Na Ukiona mwenza wako amezidisha wivu SHITUKA PENZI LENU LIKO HATARINI KUFA😭
Mara nyingi unapokuwa unaonewa wivu UTACHUNGUZWA JE WEWE UNA UKAMILIFU KWA ASILIMIA ZOTE? Ni busara kuyatunza Mapenzi kwa UAMINIFU ikiwa uko mahala Unadhani binafsi yako UNAYAPENDA💃
Wivu ukizidi unaleta hasira, Unajenga Hofu kwa moyo na MOYO ukiingiwa Hofu tu KUJITETEA KUNAHUSIKA JE MWENZIO AKIJITETEA UNAJUA ANAJITETEA JE? Mara nyingi wengi hutafuta MBADALA🤦🏾‍♂
Jihadhali na kumuingiza mwenzi wako kwenye SINTOFAHAMU Kwani muda mwingine sintofahamu zinasababisha majibu yasiyokuwa halisi, Mtu anapowaza NEGATIVITY maana yake anakwenda kuanza kukumbukia hata ule utani na kuubadili uwe ukweli mwisho wake ni MAGOMVI YASOKWISHA😭
WIVU ni UPENDO! WIVU ni UHITAJI... Pamoja na hayo yote WIVU HUSABABISHA MOYO UJUE KWAMBA MAHALA ULIPO NI SALAMA! Jitahidi kulijenga penzi lako kwa MAANA YA UAMIMIFU ili kama Ukiona unaonewa WIVU na hauna makando kando ujue kwamba DHAMANA ULIYOIJENGA KWA MWENZA WAKO IMEVUKA UWEZO WA DHAMANA YA KAWAIDA... Mapenzi yenye WIVU yana bashashaa👌
Mara nyingi ukionewa wivu ujue UKO PEKE YAKO💃
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria🙋🏻‍♂
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz