KAMA UNATAKA KUTENGENEZA AMANI KATIKA NDOA YAKO MUOMBE MUME WAKO VITU AMBAVYO ANA UWEZO NAVYO! - EDUSPORTSTZ

Latest

KAMA UNATAKA KUTENGENEZA AMANI KATIKA NDOA YAKO MUOMBE MUME WAKO VITU AMBAVYO ANA UWEZO NAVYO!

Image result for UNAINGIA KWENYE MAHUSIANO; ACHA KUMLINGANISHA WA SASA NA WAZAMANI!
Acha kumuomba mume/mpenzi wako vitu ambavyo unauhakika kuwa hana, usidhani kuwa wanaume wana miujiza ya kutafuta pesa, kwamba kuna sehemu tu akienda kuchimba anazikuta na kuja kukupa. Nikweli anahitajika kukuhudumia kama mke lakini pia anahitajika kukuhudumia kutokana na uwezo wake, lakini pia kumbuka mbali na kukuhudumia wewe kuna watu wengine nao humtegemea.
Acha kuwa mbinafsi na kutaka kupewa kila unapoomba, kumpa mume wako majukumu kwakua tu unaona rafiki zako wanafanyiwa kitu flani na wewe unataka ufanyiwe bila kuangalia kipato cha mume/mpenzi wako. Mambo si rahisi kihivyo na kumbuka mumeo mbali na kukuhudumia wewe lakini anawajibika na mipango yenu ya baadaye, kuna watoto na kuna uwekezaji anatakiwa afanye.
Kabla ya kumuomba mumeo kitu unapaswa kujiuliza maswali matatu, swali la kwanza ni je anauwezo nacho, kama jibu ni hapana acha kupoteza muda na kumuomba ili tu ukataliwe na useme unanyanyaswa, swali la pili ni je hiki kitu ni cha muhimu kwangu. Kwamba hata kama ana uwezo nacho lakini je hicho kitu kina umuhimu gani kwa wakati huo, je usipokipata itakuaje?
Kama si cha muhimu sana hembu achana nacho kwa wakati huo na elekeza akili yako katika mambo ya muhimu. Swali la tatu unalopaswa kujiuliza ni je Mume wangu ana mambo mengine yanamchanganya kwa sasa? Kwamba inawezekana ni kitu unakitaka ni muhimu lakini kama ana mambo mengine muhimu zaidi yanamsumbua basi acha.
Kwa mfano, unataka kumuomba mumeo pesa ya kushona sare ya harusi, ni muhimu sana kwa wakati huo kwani kila mtu kashona lakini kuna suala la ada za watoto, unaona kabisa ana pesa ila akilipa ada basi mtakwama. Busara si kumuambia kuhusu nguo ili apambane na hali yake ajisikie vibaya kukunyima hapana busara ni kunyamaza na kujifanya huitaki hiyo nguo!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz