AMUA AINA YA NDOA UNAYOITAKA HATA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA YENYEWE! - EDUSPORTSTZ

Latest

AMUA AINA YA NDOA UNAYOITAKA HATA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA YENYEWE!

Image result for UNAINGIA KWENYE MAHUSIANO; ACHA KUMLINGANISHA WA SASA NA WAZAMANI!
Wanawake wengi huingia katika ndoa kwa matumaini makubwa, kuna wanawake wengi ambao hawana furaha kabisa katika mahusiano yao lakini wanavumilia kwa kuamini kuwa siku nikiolewa haya yote yataisiha. Mwanamke anawaza kuwa akinioa ataacha kunipiga, akinioa ataacha kuchepuka, akinioa ataacha kunidharau na kunidhalilisha, akinioa ataanza kunihudumia kwani nitakua nishakua mke wake.
Kama uko katika mahusiano naamini kuna tabia nyingi ambazo unazivumilia kwa matumaini au malengo kuwa akinioa mambo yatakua sawa labda nitakua na furaha. Lakini haiwi hivyo, mara nyingi hua mwanamke anaponimba ushauri kuhusu tabia flani za mumewe namuuliza kama kaanza baada ya ndoa au alikua nazo kabla ya ndoa na wengi wao huniambia kuwa alikua nazo.
Hii ikimaanisha kwamba wanaume wengi hawabadiliki baada ya ndoa. Hivyo kama kuna katabia flani kawe kakubwa au kadogo ambako unakavumilia sasa kabla hajakuoa basi jua utakutana nako baada ya ndoa. Tena kwa bahati mbaya zaidi unatakiwa kujua kuwa baada ya ndoa sio tu kama utakutana nako lakini pia utakutana nako kashakua kakubwa.
Kwa mwanaume akishaoa huona kama vile kashamaliza, kuwa huyu mwanamke nimemfunga kwangu hivyo hafurukuti na haondoki hata nikimfanyia chochote. Ndiyo ambavyo wanaume wengi huamini hivi, hii ndiyo maana nakushauri kama uko kwenye mahusiano na unatamni kuingia kwenye ndoa siku moja basi hembu soma sehemu ya pili ya Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu”
Ndoa mpya ni sawa na mahusiano mapya, yanaenda wewe unavyotaka ukiamua yawe ya mateso yatakua ya mateso ukiamua yawe ya furaha yatakua ya furaha. Bei ya Kitabu ni elfu kumi tu na unatumiwa kwa Whatsapp, E-mail, au Facebook. Kukipata unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222. Irudie vizuri sehemu ya pili utakufundisha namna ya ku control mahusiano yako.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz