MWANAMKE !! HAYA NDIO MAMBO YA MSINGI UNAYOPASWA KUMFANYIA MUMEO ILI NDOA YENU ZIDI KUWA NA FURAHA NA AMANI SIKU ZOTE. - EDUSPORTSTZ

Latest

MWANAMKE !! HAYA NDIO MAMBO YA MSINGI UNAYOPASWA KUMFANYIA MUMEO ILI NDOA YENU ZIDI KUWA NA FURAHA NA AMANI SIKU ZOTE.

✍️Ndoa nyingi zimekosa uaminifu na hivyo kuna ongezeko la kupeana Talaka, ugomvi katika Ndoa na uovu mwingi katika ndoa
Ili NDOA iwe shwari, Wanandoa wote wawili wanahitaji kujua mambo muhimu.
✍️Siri ya mambo kadhaa , Siri hii ipo Kwenye Waefeso katika Bibilia "#Mke_KUMSTAHI_Mume_wake ambaye yeye Mke hufanya ili kumfanya Mumewe kumpenda na kuwa mwaminifu kwake.
✍️Japo Wanawake wengi wanaweza kuyapinga mambo fulani yeye Mke anaye fanya agizo hili katika Bibilia la kumstahi Mume wake hufanya, ameyafanya na yameinusuru ndoa yake
Hapa kuna mambo muhimu ya kufanya kuhakikisha Mumeo ni mwaminifu kwako kulingana na Waefeso 5👈 #KUMSTAHI_MUME huyu;
❤️. Usibishane naye
☑️Mke huyu anasema kuwa hajawahi bishana na Mumewe wanapokosa kuelewana. Humwendea tu kwa upole na suluhu yapatikana.
❤️Kukimya anapokasirika
☑️Nyamaza tu wakati amekasirika ili kutozidisha ugomvi. Anasema kuwa hii ndiyo mbinu nzuri zaidi ya kusuluhisha wakati Mumewe amekasirika zaidi. Humwongelesha baadaye akipoa.
❤️. Kuongea mazuri kumhusu kwa marafiki
☑️Unapokutana na marafiki zake, waonyeshe kuwa Mume wako anakufaa zaidi.
Kila Mwanaume hupena sifa. Usiwahi ongea vibaya kumhusu kwa marafiki zake.
❤️Penda Wazazi wake.
☑️Mama Mkwe kwa kiwango fulani anaweza kukufanya ubaki kwenye ndoa yako au kuiacha.
Penda tu Mama wa Mumeo na atakupenda zaidi.❤️👈🙏
❤️. Usimruhusu kijakazi wa kike kuwa karibu naye wakati wewe upo
☑️Mwanaume ni tumbo. Usikubali kiajakazi ampe chakula wakati wewe upo. Hatari sana
❤️Msifu kwa watoto wake
☑️Ni vizuri watoto wamjue kama Baba mzuri anayewapenda watoto wake.
Si vizuri kuwafanya watoto wako wamchukie Baba yao. Ataanza kukuchukia pia.
❤️Mpigie au umtumie ujumbe kuwa unammiss
☑️Mwambie maneno matamu kuwa unampenda na umemkumbuka sana. Jambo hili humfurahisha zaidi.
❤️Mtayarishie chakula kitamu zaidi
☑️Chakula kitamu humfurahisha Mume wako. Mtayarishie chakula kitamu sanasana wakati hatarajii. Suprise 😄👈
❤️Kuomba pamoja
☑️Hata Mwanaume awe mpotovi kiasi gani, hupenda kuwa na Mke mpenda maombi.
NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE 🙏 NA MALAZI YAWE SAFI 🙏 MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU ATAWAHUKUMIA ADHABU (WAEBRANIA 13: 4)




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz