Kila mtu anataka kitu kizuri, kwa wanyama kule porini majike wakati wa kuchagua dume huangalia yanapopigana na kuchagua mshindi, aliyepigwa hufukuzwa na haruhusiwi kugusa jike hata moja. Wakati mwingine hata watoto wake nao huuliwa kwakua hakuna anayetaka mbegu chafu. Sasa kwa sisi wanadamu suala la kupigana halipo na hakuna mwanamke ambaye huchagua mwanaume kwa kuangalia nguvu za kupigana.
Pamoja na ukweli huo unatakiwa kujua kua kila mwanamke, narudia kila mwanamke anapenda mwanaume ambaye anajiamini. Mwanamke husikia raha sana anapokua na mwanaume ambaye anajiamini, ambaye hana wasiwasi wasiwasi, ambaye si mtu wa kulalamika na ambaye hatishiwi na wanaume wengine. Sasa najua mke wako au mpenzi wako ana X wake, kuna ambao tunapata bahati ya kutokuwajua lakini kuna ambao mnawajua.
Kuna ambao hata wanafanya kazi pamoja, mnaishi mtaa mmoja na wengine hata nyumba moja. Kwa mwanaume anayejiamini hajali, atakachofanya ni kuweka mipaka kuwa sitaki hiki na kile, usifanye hili na lile lakini kwakua anajiamini basi anajua kuwa siwezi achwa na hata akirudiana naye basi mimi ni mwanaume nitapata mwingine sina haja ya kuwa na wasiwasi.
Lakini mwanaume kama unataka kumpoteza huyo mpenzi wako basi acha kujiamini, tishiwa na uwepo wa X wake, utamfanya awaze mara mbili hivi nilimkubali nini huyu mtu? Kama wewe ni wale wanaume ambao kutwa kukagua simu yake, ukimuona hata akipishana na jamaa mko mjini mnakutana na jamaa umenuna hutaki hata salamu, ametoka kidogo na marafiki unaanza kuulizia kama yuko na X wake na mambo kama hayo.
Yaani hujiamini kila wakati unahisi unasalitiwa ndugu yangu kinachofuatia ni kusalitiwa kweli na kuja kuachwa. Iko hivi unapokua na wivu wa ajabu ajabu kuhusu X wake basi utakuta kila ugomvi mnaokua nao ni kuhusu huyo X wake inawezekana hata alishamsahau, ni mwanaume ambaye alimuumiza sana hivyo hataki kumkumbuka lakini kila siku wewe unamtajataja mpaka basi.
Humpi nafasi ya kumsahau, lakini sasa anaanza kukulinganisha na huyo X, si unamtaja taja anaanza kuwaza mbona yeye hakua hivyo, mbona yeye hakuwa hivi mbona hivi na vile. Yaani ni kama unamlazimisha mwanamke kummiss X wake, kwamba anawaza mbona haka kajitu hakajiamini hivi, kana kasoro gani. Kwamba kikawaida wanaume tunategemewa kujiamini hivyo unapokua hujiamini mtu huhisi una kasoro.
Unamlazimisha ananza kuwaza au maumbile yake yako hovyo, yaani anayona kila siku lakini kwakua hujiamini basi anayafikiria mara mbili, anawaza au huwezi kazi, au hiki au kile. Sasa badala ya kutafuta vitu vizuri kwako vya kumalazimisha akupende wewe unamlazimisha kutafuta kasoro zako. Ndiyo hutakiwi kumpa uhuru wa kuwasiliana naye eti wanachat sijui nini hapana huo ni ujinga.
Hata kama wana mtoto inamaana ampigie kusalimia mara moja au kunapokua na shida lakini si kupiga kila mara na suala la kuchat hilo muambie kabisa nikikuona unachat na X wako ndugu yangu nakuitia bodaboda na kurudisha kwake (wanaume tunajuana nini kinatokea ukimuacha achat chat naye). Ajue hivyo kuna mipaka lakini lisiwe ni suala la kila siku kumzungumzia na kumlalamikia.
Ukiona kama kila siku mnamzungumzia huyo X wake, ukiona kama kila kitu anachofanya wewe nilazima umtaje huyo X wake, ukiona kuwa huwezi kufanya kitu bila kujilinganisha naye, hata zawadi unajilinganisha basi jua kwanza hujiamini, pili ni jambo la wakati tu utamlazimisha amfuate kwani ni kama unamuambia kuwa mimi sitoshi ikilinganisha na jamaa yako wa zamani unapoteza muda tu na mimi!
No comments:
Post a Comment