MOURINHO AMFUNGUKIA POGBA - EDUSPORTSTZ

Latest

MOURINHO AMFUNGUKIA POGBA

Mourinho adai pogba anaelewa kilichomfanya kufanya vyema kombe la dunia
Mourinho adai pogba anaelewa kilichomfanya kufanya vizuri katika kombe la dunia

 Mourinho kocha mkuu wa club ya Man United amesema ana matumaini kuwa mchezaji wake kutoka ufaransa Paul Pogba anaelewa kuhusu ni kwanini alicheza vizuri zaidi wakati wa mechi za Kombe la Dunia.

Kiungo hiyo wa safu ya kati wa Red Devils alifunga wakati Ufaransa waliishinda Croatia mabao 4-2 na kushinda Kombe la Dunia kwa mara ya pili.

Mourinho alisema Pogba mwenye miaka 25 alionyesha mchezo mzuri sana kwenye mechi tatu za mwisho nchini Urusi.

"Ni yeye mwenyewe kufahamu ni kwa nini alicheza vizuri, hasa wakati wa awamu ya pili ya mashindano," alisema Mourinho.

Pogba alijiunga na United kwa pauni milioni 89 mwezi Agosti mwaka 2016, lakin akawa anachwa nje wakati wa mechi za msimu wa mwaka 2017-2018.

Aliachwa nje ya kikosi cha kwanza katika mechi zote wakati wa awamu za timu 16 za mwisho ambapo United ilishindwa na Sevilla.

Baada ya ushindi wa Ufaransa wa siku ya Jumapili beki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand alisema "ni jukumu la Mourinho kumleta Pogba aliyekuwa kwenye Kombe la Dunia, alipitia mitihani migumu kwenye safu ya kati.

Huku Red Devil ikisafiri kwenda Marekani kwa safari ya maandalizi Pogba amebaki kupumzika.

Mourinho akizungumza  huko Los Angeles,  alisema, "nilimfanyia Pogba kile nilichowafanyia wachezaji wengine.

Nilituma ujumbe mzuri kabla ya Kombe la Dunia na wakati wa Kombe la Dunia sikumsumbua yeyote, Walihitaji kuangazi tu kazi ya timu zao za kitaifa.

Mourinho alisema kipa David de Gea, kiungo wa kati Nemanja Matic na mchezaji mpya Fred watajiunga na kikosi hicho wiki ijayo.

Mshambuliaji Alexis Sanchez kujiuanga kwenye ziara hiyo baada ya kukosa kupata visa.

Chanzo. Bbc swahili


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz