SIMBA YATAFUNWA BILA HURUMA - EDUSPORTSTZ

Latest

SIMBA YATAFUNWA BILA HURUMA

 
Klabu ya Gormahia ya nchini Kenya imefanikiwa kuchukua ubingwa wa michuano ya Sportpesa kwa kuifunga klabu ya Simba ya Tanzania goli 2-0.
Wachezaji wa Klabu ya Gormahia ya nchini Kenya wakishangilja kuchukua ubingwa wa michuano ya Sportpesa baada ya  kuifunga klabu ya Simba ya Tanzania Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Gor Mahia walitawala zaidi mchezo wakiwa na kikosi chao kamili huku Simba wakipata wakati mgumu kutengeneza nafasi za kufunga. 
Gor Mahia wamejipatia mabao yao kupitia kwa Mshambuliaji wao hatari, Medy Kagere aliyefunga la kwanza katika dakika ya 6 tu ya mchezo na kufanya kipindi cha kwanza kiende kwa bao 1-0. 
Kipindi cha pili kilianza tena kwa Gor Mahia kuzidi kulisakama lango la Simba wakionesha njaa ya kupata goli jingine ambapo mnamo dakika ya 54, Tuyisenga alifunga bao la pili kwa kumalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka kulia mwa Uwanja na kumuacha Kipa Aishi Manula akiwa hana cha kufanya.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Gormahia kuchukua ubingwa huo baada ya mwaka jana kuchukua ubingwa huo ambao mashindano yake yalifanyika nchini Tanzania.

Gormahia wamejikatia tiketi ya kwendaGoodison Park nchini uingereza kucheza dhidi ya Everton.

Mchezo huo umekamilika kwa mabao 2-0 


Chanzo: Mtila blog
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz