ORODHA MPYA YA WANAMICHEZO MATAJIRI DUNIANI - EDUSPORTSTZ

Latest

ORODHA MPYA YA WANAMICHEZO MATAJIRI DUNIANI


Mwanamasumbwi wa Marekani Floyd Mayweather ametetea taji lake katika porodha ya Forbes ya wanamichezo wanaopata mapato ya juu zaidi duniani.

Alijipatia kipato cha $275m (£205m) katika mechi yake ya masumbwi mwezi Agosti dhidi ya nyota wa UFC star Conor McGregor, ambaye yuko nambari nne katika orodha ya jarida hilo la biashara nchini Marekani.

Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akiorodheshwa wa kwanza katika kipindi cha miaka 2 iliopita sasa ni wa tatu huku Lionel Messi akichukua wadhfa wa pili kwa tofauti ndogo.

La kushangaza ni kwamba hakuna wanawake katika orodha hiyo baada ya mwanamke wa pekee katika orodha hiyo Serena Williams kutoorodheshwa.

Wachezaji 100 bora walijipatia jumla ya $3.8bn, ikiwa ni nyongeza ya asilimia 23 kutoka mwaka uliopita ,Forbes ilisema

Dereva wa magari ya F1 Lewis Hamilton ndio mwanamichezo Muingereza anayelipwa kipato cha juu cha $51m akiwa nambari 12.

Mayweather ambaye jina lake la utani ni Money-aliongeza kipato chake cha michezo kwa $10m

"Mechi kubwa kati yake na McGregor 2017 iliwasaidia Mayweather na McGregor kujipatia pato la jumla ya $400m'' , alisema Kurt Badenhausen, Mhariri mkuu wa jarida wa Forbes Media.

"Lakini wachezaji wa mpira wa vikapu wametawala orodha ya wanamichezo 100 kufuatia kuongezwa kwa mishahara yao inayotokana na kandarasi ya maouyesho ya runinga ya $24bn

Aliongezea: "Orodha ya Forbes' ya wachezaji wanaopata mapato ya juu imejaa wanaume. lakini kumekuwa na mchezaji mmoja wa kike ambaye alifuzu baada ya orodha hiyo kuongezwa hadi majina 50 2010.


Wanamichezo 10 tajiri zaidi duniani.


  1. Floyd Mayweather - Ndondi ($285m)
  2. Lionel Messi - Kandanda ($111m)
  3. Cristiano Ronaldo -Kandanda($108m)
  4. Conor McGregor - Karate, judo na Ndondi ($99m)
  5. Neymar - kandanda ($90m)
  6. LeBron James - Kikapu ($85,5m)
  7. Roger Federer - Tenisi ($77.2m)
  8. Stephen Curry - Kikapu ($76.9m)
  9. Matt Ryan - Soka ya Marekani ($67.3m)
  10. Matthew Stafford - Soka ya Marekani ($59.5m)


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz