Mpira wa miguu |
1.Manchester United wana nia ya kuipa Real Madrid ofa ya pauni milioni 70 kwa kiungo wake wa safu ya kati raia wa Uhispania mwenye miaka 26 Isco. (Mundo Deportivo - in Spanish)
2Mo Salah: Ilikuwaje akawa mchezaji nyota?
Mshambulizi wa Chelsea Michy Batshuayi anasema hawezi kuamua hadi baada ya kombe la dunia ikiwa atarudi Stamford Bridge. Rais huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 alitumikia duru ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo huko Borussia Dortmund.(Evening Standard)
3.Tottenham itaiomba Manchester United mshambuliaji raia wa Ufaransa Anthony Martial 22, ikiwa mlinzi raia wa Ubelgiji Toby Alderweireld, 29 atahamia Tottenham.
4.Chelsea inaweza kumtoa mshambulili raia wa Uhuspania Alvaro Morata 25, kwa Inter Milan ili kumdilisha na mshambulizi raia wa Argentina Mauro Icardi, 25. (Il Messaggero, via Mail)
Nani atawika fainali Kiev kati ya Salah, Ronaldo na Milner?
Arsenal na Chelsea watapata ushindani kutoka Napoli na Borussia Dortmund kumpata kiungo wa kati wa Nice na Ivory Coast Jean-Michael Seri, 26. (Sun)
5.Maajenti wa Marco Asensio wanasema Real Madrid wamekataa ofa mbili kutoka klabu za Premier League za thamani ya hadi pauni milioni 130 kwa mshambulizi mhispania mwenye miaka 22 ambaye amehusishwa na Manchester United na Chelsea. (Independent)
6.Mashabiki wa Liverpool watinga Kiev
West Ham wako nafasi nzuri kumsaini mlinzi wa Barcelona Marlon. Mbrazili hiyo wa miaka 22 ambaye anacheza kwa mkopo wa miaka miwili na klabua Nice pia anawindwa na Leicester. (Mundo Deportivo - in Spanish)
7.Manchester City wanataka kuwasaini kiungo wa kati wa Italia Jorginho kutoka Napoli, wing'a wa Leicester raia wa Algeria Riyad Mahrez, 27 na mshambuliaji wa Bayer Leverkusen raia wa Jamaica Leon Bailey. (Manchester Evening News)
8.Manchester United walikwa na matumaini ya kumsaini beki wa Juvemntus raia wa Brazil Alex Sandro, lakini mchezaji huyo wa miak 27 anatarajiwa kufanya mazungumzo wiki ijayo kubaki nchini Italia. (Mirror)
9.Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameweka tayari pauni milioni 30 kumnunua beki wa Valencia Joao Cancelo. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ureno mwenye umri wa maika 23 akiwa Inter Milan msimu uliopita kwa mkopo. (Mirror)
10.Chelsea wanakabiliwa na usindani kutoka kwa Zenit St Petersburg ya Urusi kwa meneja Maurizio Sarri. Meneja huyo wa Napoli anaonwa kama anayeweza kuchukua mahala pake Antonio Conte huko Stamford Bridge. (Guardian)
11.Kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, 24, atajiunga na Juventus mwisho mwa mwezi huu huku mkurugenzi mkuu wa mabingwa hao wa Italia Giuseppe Marotta akisema anataka kukamilisha mpango huo ndani ya siku 10. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
12.Manchester United wana nia kulipa pauni milioni 79 kumsaini wing'a Douglas Costa kutoka Bayern Munich. Mchezaji huyo raia wa Brazil mwennye miaka 27 yuko kwa mkopo huko Juventus na mabingwa hao wa Italia wana uamuzi wa kumsaini kabisa. (Sun)
13.Kwingineko United hawama uhakika ikiwa watamwinda kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, baada ya klabu hiyo ya Italia kutangaza bei ya mchezaji huo kuwa pauni milioni 87.5 kwa raia huyo Serbia. (Mail)
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au
kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
No comments:
Post a Comment