SAFARI YA KICHUYA TP MAZEMBE IMEIVA - EDUSPORTSTZ

Latest

SAFARI YA KICHUYA TP MAZEMBE IMEIVA

Shiza ramadhan kichuya amekuwa katika kiwango bora katika misimu yote ambayo amekuwa simba toka asajiliwe. Ni moja ya wachezaji waliochangia simba kuwa mabingwa huku akiwa amechangia magoli 20 katika msimu unaelekea kumalizika mpaka sasa. 

 Lakini mkataba wa kichuya unaenda kumalizika mwaka huu pale msimbazi na hatma ya kubaki au kuondoka simba ipo mikononi mwake kwani lengo lake ni kwenda kucheza soka la kulipwa nje Baba mzazi wa kichuya amenukuliwa akisema anaona muda wa kucheza soka la ndani kwa mwanawe umeisha ni muda sahihi wa kwenda nje kwa ajili ya kujaribu bahati yake huko.

 Mkuu wa habari na mawasiliano simba haji sunday manara alihojiwa swali hilo kupitia kipindi cha leo tena kinachorushwa na clouds na alijibu kama ifuatavyo "ni kweli shiza kichuya mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huu na tunapenda kubaki nae ila pia tutaangalia kama atakubali kuboreshewa maslahi yake, kwani bado klabu inampenda na ana mashabiki wengi pale msimbazi.
Ila kama ataamua kwenda nje kucheza soka sisi kama klabu hatuwezi kumzuia kwa maslahi yake, familia pamoja na nchi yake. Tp mazembe ni moja ya timu zinazovutiwa na kichuya kwa hiyo pengine anaweza kupita kwenye mlango ambao samatta alipitia.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz