TETESI ZA USAJILI LEO BARANI ULAYA MAY 23 - EDUSPORTSTZ

Latest

TETESI ZA USAJILI LEO BARANI ULAYA MAY 23


Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anatathmini kumwinda mchezaji wa Ajax raia wa Uholanzi Matthijs de Ligt,18. (Guardian)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anafikiria kuchukua likizo kutoka kandanda ikiwa atafutwa na klabu hiyo. Telegraph)Anthony Martial
Manchester United wana nia ya kusikiliza ofa kwa mshambuliaji raia wa Ufaransa Anthony Martial, 22, lakini wako makini wasije wakamuuza kwenda klabu pinzani ya England. (Mail)

AC Milan wana mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Chelsea rai wa Uhispania Alvaro Morata, 25. (Sky Italia - in Italian)Unai Emery

Unai Emery hatakuwa na ushawishi katika kuwanunua na kuwauza wachezaji wakati atateuliwa meneja wa Arsenal. (Mirror)

Emery ana nia ya kumweka kiungo wa kati Aaron Ramsey, 27, katika mipango yake licha mchezaji huyo kuhusishwa na mpango wa kukihama klabu hiyo. (Sky Sports)Mikel Arteta

Kocha msaidizi Mikel Arteta anafanya makubaliano na Manchester City baada ya kushindwa kupata kazi huko Arsenal. (Telegraph)

Arsenal wanapanga kumsaini kiungo wa kati wa Nice raia wa Ivory Coast Jean Michael Seri, 26. (Mail)

Arsenal, Chelsea na Everton wote wanammezea mate mlinzi wa Hamburg mjerumani Josha Vagnoman 17. (ESPN)Carlo Ancelotti


Meneja wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Carlo Ancelotti amefanya mazungumzo na raia wa Napoli kuhusu kuchukua mahala pake Maurizio Sarri. (Sky Sports)

Swansea wamefanya mazungumzo na meneja wa Ostersunds FK, Graham Potter kuhusu nafasi iliyo wazi wa umeneja. (Mail)Moussa Sissako

Meneja wa New York City na kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira amekana ripoti kuwa anapanga kujiunga an Nice kama meneja. (Goal)

Brighton wanakaribia kumsaini mlinzi wa Paris St-Germain raia wa Mali Moussa Sissako, 17. (RMC- via Mirror)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, amesema wazi wazi anatataka kuondoka Real Madrid msimu huu wa joto , mwaka mmoja baada ya Mbrazil huyo kujiunga na mabingwa hao wa Ufaransa. (Goal)

Chelsea wamemuorodhesha mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 29, miongoni mwa wanaowataka kuwasajili msimu huu. (Telegraph)

Manchester United wanamatamanio ya kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Willian, 29, msimu huu wa uhamisho. (Sky Sports)

Lakini Manchester United wako tayari kujiondoa kwa uhamisho wa £53m wa Shakhtar Donetsk na kiungo wa kati wa Brazil Fred ,25. (Metro)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Manchester United Anthony Martial, 22, ananyemelewa na mahasimu wao wa ligi ya Premia Tottenham. (London Evening Standard)

Barcelona wanapanga kusamjili mshambuliaji wa Spurs Reo Griffiths katika uhamisho wa msimu huu wa joto. (Star)
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz